Jumanne, 27 Mei 2014

SERIKALI YAJIPANGA KUKUZA UELWA KWA WANANCHI KUSIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

Timothy Marko.
Katika kuhakikisha  wananchi wanapata  uelewa wa maswala ya utunzaji mazingira katika maeneo yao  serikali kupitia wizara inayohusiana na mazingira imepanga kutuoa elimu pamoja na mafunzo  yajinsi ya kukabiliana na  maswala yahusuyo tabia yanchi .
Akizungumza leo jijini na waandishi wa habari waziri wamazingira ofisi ya makamu wa Rais Binilith Mahenge amesema kuwa hali ya madiliko ya tabia yanchi yanasababishwa na ongezeko la gesi joto inayotokana na  shughuli za maendeleo ya binadamu .
‘’Mabadiliko ya shughuli za binadamu ndio chanzo cha ongezeko la joto duniani ambapo mabadiliko hayo hutokea baada ya miaka 30 hii ni kutokana nauzalishwaji wagesi duniani ambapo hali hii husababishwa na shughuli za uzalishwaji wa matumizi yasiyo endelevu ya nishati kutoka viwandani,usafirishaji,shughuli zakilimo chenye matumizi makubwa ya mbolea,ukataji miti ovyo husan katika nchi zilizo endelea’’alisema Binilith Mahenge.
Waziri Binith Mahenge alisema kuwa kiwango chaukataji miti katika nchi zinazoendelea zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa katika uhalibifu wa wazingira .
Akizungumza kuhusiana  na siku ya maadhimisho ya mazingira duniani inayotarajia kufanyika 5juni mwaka huu waziri Mahenge amesema kuwa maadhimisho yasiku yamazingira yanatajiwa kufanyika mkoani mwanza ikiwa nakauli mbiu ya ‘’chukua hatua namna ya kukabiliana na tabia yanchi ambapo awataka wananchi kwakudhibiti uchomwaji wa misitu ya asili.
‘’katika kutoa mchango wetu wakukabiliana na mabadiliko yatabia ya nchi tunasisitiza juu ya jamii kuondokana na uchomwaji wamisitu na kuhimiza upandaji wamiti katika vyanzo vya maji ilikuweza kudhibiti uhalibifu wamazingira katika ardhi nakuzuia nchi kuwa jangwa ‘’alisema waziri Mahenge.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni