Jumatatu, 26 Mei 2014

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAJIZATITI KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

Timothy  Marko
Katika  kuhahikisha  sekta ya afya inaimarika nchini  hosipitali kuu ya taifa Muhimbili imezindua  mpango  maluumu wakuboresha huduma zake katika hospitali hiyo ujulikanao  awamu yatatu ya moi  ikijumuisha uboreshaji wa majengo katika hospitali hiyo.
Akizungumza jijini leo  Meneja uhusiano wa muhimbili (MOI) Almas  Juma amesema kuwa  kumekuwa na malamiko kwa baadhi ya wananchi wanaofika katika hospitali hiyo kuhusiana na huduma  zinazo tolewa na hospitali hiyo kuwa zipo katika kiwangokisicho ridhisha hivyo tume amua kujenga  jengo  jipya ambalo litaweza kuwa  na vitanda 380 .
‘’tutakuwa najengo jipya ambalo litakuwa navitanda 380 hadi hivi sasa tunaweza kuhudumia vitanda 159 ambapo uboreshwaji huu utaenda sambamba na miundo mbinu ya hospitali kikiwemo maabara na vifaa vyake ‘’alisema Almas Juma.
Almas juma alisema kuwa uboreshwaji wamiundombinu ya hospitali sambamba na uboreshwaji wa huduma katika hospitali hiyo kutaweza kupunguza gharama za wananchi kutibiwa nje ya nchi ambapo serikali huingia gharama kuwa katika kuwa safirisha wagonjwa.
Alisema kuwa huduma nyingi za upasuaji wa mifupa hufanyika hapa hapa nchini ambapo baadhi ya wataalamu wa huduma hiyo wanapatikana hapa nchini .
‘’asilimia 80ya operesheni ya mifupa inafanyika hapa nchini ambapo  kutokana naukosefu wavifaa kama city scan MRI’’aliongeza Almas.
Aliongeza kuwa hospitali yake inaupungufu wa madakitari 70 ambapo baadhi yao huenda katika nchi za nje ilkuweza  kufanya kazi .
Alisisitiza kuwa hospitali hiyo yataifa imekuwa yakwanza katika kutoa huduma kwa njia zakisasa zaidi kwa kutumia tenknolojia  .’’hospitahii imekuwa yakwanza ambapo hadi sasa tunavyo vitanda 180 hadi kufikia 159 hatimaye baada ya mabadiliko  ya WHO ambapo kila wodi inawagojwa 35’’alisema Almas.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni