WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA Charles Mwijage . |
WAKATI Tanzania ikielekea katika uchumi wa viwanda ,imebainishwa kuwa uanziashwaji naukuzaji waviwanda vidogo vidogo ndivyo vitakavyo chochea ukuwaji wa uchumi kupitia sekta hiyo .
Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Waziri wa viwanda na Biashara Charles Mwijage wakati akizindua ripoti ya sensa ya viwanda ambapo alibainisha kuwa Tanzania haipo katika halimbaya ya sekta hiyo ambapo alibainisha kuwa Mkoa wa Dar es salaam ndio unaongoza kwakuwa naviwanda vingi ambapo jumla yaviwanda 7444 vipo katika mkoa huo ikifuatiwa namkoa wamara wenye viwanda 3,549 .
''Taswira inaonesha kuwa maendeleo yaviwanda nchini Tanzania kama nchi nyingine yanatokana nakuweka nguvu katika sekta yaviwanda vidovidogo sana navidogo faida za sektahii haitaji elimu kubwa namtaji mkubwa hivyo vinaweza kuanzishwa katika eneo lolote katika nchi yetu ''Amesema Waziri waviwanda na biashara Charles Mwijage .
Waziri Mwijage amesema kuwa sekta yaviwanda inatoa mwanya mkubwa kwa vijana na wanawake kuanzisha viwanda nakujiajiri ambapo wasingeweza kupata katika sekta nyingine zinazotoa ajira .
Alisema Takwimu zinaonesha viwanda vidogo vidogo ndivyo vinavyongeza thamani ya mazao hali ambayo humpatia kipato zaidi mzalishaji nakupunguza hasara baada ya mavuno kama katika mikoa ya Mara yenyeviwanda 3,549 Ruvuma yenyeviwanda 3,477 .
''VIWANDA vidogo vidogo ndio huongeza thamani ya mazao hali inayochangia kumpatia kipato zaidi mzalishaji nakupunguza hasara yamavuno katika mikoa mbalimbali ikiwemo ruvuma na Dar es salaam ''Aliongeza .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni