Timothy Marko .
HALI kuwepo kwa maadhimisho ya siku yakumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na kuwepo kwa Mapumziko ya wiki marefu imelezwa ndio chanzo kikuu cha mauizo ya hisa kushuka kwa asilimia 91 kwa wiki hii .
Akizungumza na waandishi wa Habari Afisa Mwandamizi wa Soko la hisa Mary Kinabo jijini Dar es salaam amesema kutokana namapumziko marefu ya mwisho wa wiki yalioyo ambatana na maadhimisho yakumbukumbu ya Kifo cha hayati Mwalimu nyerere yameshachangia kushuka kwamauzo yahisa sokoni hapo kutoka bilioni 32.5 hadi kufikia bilioni 3 kwa wiki hii.
''Wakati hali hii ikitokea tunaona mojakwamoja mauzo yetu yameshuka hadi kufikia bilioni 3 kutoka bilioni 32.5 wakati kampuni zinazo ongoza kwamauzo nipamoja na CRDB (53%) ikifuatiwa kampuni ya TCC (41%) wakati TBL Ikishika nafasi yatatu kwamauzo kwa asilimia (4%)''Alisema Afisa Mwandamizi wa DSE Mary Kinabo .
Kinabo amesema kuwa wakati Benki ya Crdb ikiongoza kwa mauzo katika Soko hilo ukubwa mtaji wa wasoko umeshuka kwa asilimia tatu kutoka trioni 21.49 hadi trioni20.8 huku mtaji wamakampuni yandani ukibakikatika kiwango cha awali .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni