Timothy
Marko.
IMELEZWA
kuwa magonjwa mengi yasiyo ambukiza
yanatokana na kuwepo kwa tabia hatarishi ikiwemo kulavyakula visivyozingata
virutubisho sahihi nakwakati sahihi .
Hayo
yamebainishwa leo na Mkurugenzi wa Taasisi ya impact afya Dk.Fred Mushiri
wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo amesema
magonjwa mengi yasiyo ambukiza yatokana na mtindo wa maisha ikiwemo kula
vyakula hivyo pasipo kufanya mazoezi .
‘’Suala zima
la lishe na kutofanya mazoezi sio kitu kizuri kwani nihatari kwa afya hali
inayochangia ongezeko lauzito ,lishe bora ni ile kiasi gani na kwawakati gani ‘’Alisema
Dk.Fred Mushiri .
Dk Mushiri
alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa ongezeko la watu wanaokabiliwa namagonjwa
yasiyo ambukiza kwa kiasi kikubwa taasisi yake ya impact afya imeanza kutoa
elimu kwa taasisi mbalimbali kuweza kutenga muda kwa wafanyakazi wao muda wa
kufanya mazoezi.
Alisema
ilikuweza kukabiliana natatizo lamagonjwa yasiyo ambukiza jamii lazima itenge
muda wamazoezi ilikuweza kuondokana namsongo wa mawazo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni