Jumatano, 7 Septemba 2016

SERIKALI KUSHIRIKIANA WHO KATIKA KUTOKOMEZA TAKA HATARISHI JIJINI .

Tokeo la picha la wizara ya afya
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII


Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha suala la Taka hatarishi linadhibitiwa ipasavyo serikali kupitia wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto imesema kuwa itaendesha oparesheni ya uteketezaji wa taka hizo kuanzia kesho .

Akizungumza na waandishi wahabari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Afya na kinga wa wizarahiyo Neema Rubanyila amesemakuwa mradi huo wakuteketeza taka hatarishi zinzotoka katika vituo mbalimbali vya afya umelenga hospitali tano zilizopo katika mkoa wa Dar es salaam ikiwemo Hospitali ya taifa ya  Muhimbili .

‘’Mradi huu wa kuteketeza Taka hatarishi zinzotoka hospitali mbambali ikiwemo hospitali ya muhimbili unalenga hospitali tano hadi kumi nambili katika mkoa wa Dar es salaam ,juhudi za kutekeza taka hatarishi zilikuwepo tangia mwaka 2011 lakini mradi huu umekuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wavitendea kazi ‘’Alisema Mkurugenzi wa Kinga wizara ya Afya Neema Rubanyila .

Mkurugenzi Rubanyila alisema kuwa moja yataka hatarishi zinazotoka katika hospitali nipamoja nataka zenye vimelea vya madini ya Mecyuri madini hayo huwa na athari kubwa kwabinadamu hivyo yanahitaji umakini mkubwa katika kuteketeza taka za jamii hiyo .

Alisema kuwa Mradi huo wakuteteza taka hatarishi unafadhiliwa na shirika la umoja wamataifa linaloshughulikia masuala ya afya (WHO)pamoja na Shirika lamaendeleo la umoja wa mataifa pamoja nashirika la CDC la kutoka nchini Marekani .

‘’Mradi huu nimuhimu sana kwa mstakabali wananchi wa Dar es salaam nanchi nzima kwa ujumla kwani taka hizi zimekuwa nihatarishi kwani taka aina za mecyuri huweza kuleta madhara kwa wananchi ikiwemo kusababisha ulemavu wangozi kutokana na madini yake kuwa nathari kwa jamii’’Aliongeza Rubanyila .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni