Jumatano, 28 Septemba 2016

MIFUKO YAHIFADHI YA JAMII YA WAKWAMISHA WATANZANIA KUPATA HUDUMA ZA AFYA .

Tokeo la picha la SSRA

mamlaka ya mifuko yajamii nchini




Timothy Marko.
IMEBANIKA kuwa zaidi ya asilimia 91ya watanzania hawajajiunga namifuko ya hifadhi yajamii suala ambalolimewafanya watazaniawengi kutopata huduma zinazotolewa namifuko hiyo ikiwemo huduma ya matibabu katika vituo vya afya .

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya hifadhi yajamii nchini (SSRA) Onorius Njole wakati akizungumza katika ufunguzi wa warsha yasiku moja ya waandishi wa habari iliyokuwa ikilenga kukuza uelewa juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

‘’ambapo kiwango hiki nikidogo ukilinganisha nauhitaji wa huduma za hifadhi yajamii ,hali hii imechangiwa kutokuwa na uelewa mdogo watanzania juu ya umuhimu wa mifuko yauhifadhi wa jamii ‘’Alisema Mkurugenzi wa Sheria Onorius Njole .

Mkurugenzi wa Sheria Njole amesema kuwa kumekuwa namalamiko juu ya fao lakujitoa hivyo kutokana nakuwepo kwa malalamiko hayo ,mamlaka hiyo imeanzisha fao lijulikanalo kama fao upotevu wa ajira .

Amesema katika kipindi cha mwaka huu jumla shilingi trioni 1.7 zimeweza kupokelewa na waajiri kama michango ya waajiriwa kama pensheni katika mifuko mbali mbali nchini.

‘’Taasisi za serikali zimekuwa zikikabliwa madeni mengi hali inayochan giwa kutowasilisha michango yawanachama wao kwa wakati ambapo imebainika zaidi 10 ya taasisi za umma ndizo zinazowaslisha michango yao kwa wakati ‘’ Aliongeza Njole .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni