mamlaka ya mifuko yajamii nchini |
Timothy
Marko.
IMEBANIKA
kuwa zaidi ya asilimia 91ya watanzania hawajajiunga namifuko ya hifadhi yajamii
suala ambalolimewafanya watazaniawengi kutopata huduma zinazotolewa namifuko
hiyo ikiwemo huduma ya matibabu katika vituo vya afya .
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya hifadhi yajamii nchini
(SSRA) Onorius Njole wakati akizungumza katika ufunguzi wa warsha yasiku moja
ya waandishi wa habari iliyokuwa ikilenga kukuza uelewa juu ya mifuko ya
hifadhi ya jamii.
‘’ambapo
kiwango hiki nikidogo ukilinganisha nauhitaji wa huduma za hifadhi yajamii
,hali hii imechangiwa kutokuwa na uelewa mdogo watanzania juu ya umuhimu wa
mifuko yauhifadhi wa jamii ‘’Alisema Mkurugenzi wa Sheria Onorius Njole .
Mkurugenzi
wa Sheria Njole amesema kuwa kumekuwa namalamiko juu ya fao lakujitoa hivyo
kutokana nakuwepo kwa malalamiko hayo ,mamlaka hiyo imeanzisha fao lijulikanalo
kama fao upotevu wa ajira .
Amesema
katika kipindi cha mwaka huu jumla shilingi trioni 1.7 zimeweza kupokelewa na
waajiri kama michango ya waajiriwa kama pensheni katika mifuko mbali mbali
nchini.
‘’Taasisi za
serikali zimekuwa zikikabliwa madeni mengi hali inayochan giwa kutowasilisha
michango yawanachama wao kwa wakati ambapo imebainika zaidi 10 ya taasisi za
umma ndizo zinazowaslisha michango yao kwa wakati ‘’ Aliongeza Njole .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni