Meneja Mauzo na Biashara DSE Patrick MUSUSA |
Timothy
Marko.
IDADI ya mauzo
ya hisa katika soko la Dar es salaam Stock
Exchange (DSE) imeongezeka kwa asilimia
75 kutoka shilingi bilioni 2.2 hadi kufikia bilioni 3.8 huku ikiwa mtaji wa
makampuni ya ndani umeshuka kwa asilimia 8.5 kutoka trioni 20 hadi kufikia
trioni 20.8 kwa wiki iliyopita .
Akizungumza
na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Menejamiradi Masoko na Biashara
Patrick Mususa amesema kuwa Hali hiyo imechangiwa na shughuli mabalimbali za
manunuzi na kuuza hisa zao baada ya soko hilo kukuza uelewa ikiwemo kutumia
vyombo vya habari juu yaumuhimu wa hisa katika kukuza uchumi .
‘’Wakati huo
huo Makapuni yanayo ongoza katika kuuza hisa katika soko lahisa nipamoja CRDB
kwa asilimia 28 ,DSE Asilimia 22 huku kampuni ya sigara nchini ya TCC ikishika
nafasi yatatu kwa asilimia 21 kwa kwa kununuliwa hisa zake ‘’Alisema Meneja
Miradi na Biashara Patrick Mususa .
Mususa
alisema kuwa wakati mauzo ya hisa yaikiongezeka kwa asilimia 75 sekta ya
viwanda imeshuka kutokana na kupungua kwa kaunta ya kampuni ya bia nchini (TBL)
kwa asilimia 2.6
Alisema kuwa
Sekta yakibenki imeonekana kushuka kutokana na ongezeko lahisa katika kaunta ya
soko lahisa kushuka kwa asilimia 0.82
‘’Sambamba
na hilo pia katika soko letu kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa wanafunzi hasa
katika kipindi cha mwaka jana ambapo wanafunzi wengi walijitokeza kununua hisa
kwa asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka huu ambapo mkoa wa Arusha ndio umekwa
ukiongoza kwa wanafunzi kuwekeza kupitia soko la Hisa ‘’ Aliongeza Mususa .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni