Alhamisi, 14 Julai 2016

MWANAZUONI AWAONYA WANAOMKEJELI RAIS MAGUFULI.



Timothy Marko.
WANASIASA wametakiwa kutobeza juhudi za Rais  Dk.Jonh Magufuli za kuwaletea maendeleo badala yake wamsaidie kufanya kazi yenye kuleta  mafanikio yenye tija  nchini.

Hayo yamebainishwa na mwanazuoni DK.Haruni Kondo wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika uzinduzi wa kitabu cha uongozi wa awamu yatano na hatima ya nchi yetu kilicho andikwa na mwanazuoni huyo , mapema hii leo jijini Dar es salam, ambapo amesema kuwa Rais Magufuli amekuwa akijikita katika misingi ya muasisi wa taifa hili Mwalimu Nyerere.

‘’Watanzania tunapaswa kuwa makini na kukataa hadaa na propaganda za baadhi ya wanasiasa uchwara wabinafsi wenye uchu na uroho wa madaraka ‘’Alisema Mwanazuoni DK.Haruni Kondo.

Mwanazuoni Kondo alisema kuwa wanasiasa ,wasomi watumishi wa umma na wafanyabishara na viongozi wadini wamekumbwa na ugonjwa wa husuda .

Alisema kuwa Wanasiasa pamoja na viongozi wadini wanapandikiza chuki kwa wananchi hao nisumu kwa mstakabali wa nchi yeyote ile .

‘’Watu wa aina hii wanapandikiza chuki wana maradhi wanaweza kuleta mpasuko nakisha kuleta vurugu na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi zao ‘’aliongeza Mwanazuoni KONDO.  


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni