Ijumaa, 15 Julai 2016

MABENKI 30 KUSHIRIKI MAONESHO YA TAASISI ZA KIFEDHA JULAI 27

MWANDAJI WA MASHINDANO YA KIBENKI LEO NYADUGA.



Timothy Marko.
Zaidi ya Mabenki 30  hapa nchini yanatarajia kushiriki katika maonyesho ya Kifedha  yatayo shirikisha sekta binafsi na Taasisi za Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leojijini  mwandaji wa maonesho hayo yakibenki Leo Nyanduga amesemakuwa katika maonesho hayo yanayotarajiwa kufanyika julai 27-29 mlimani city  yanalenga kutoa  kuwajulisha wananchi mbalimbali juu ya huduma zitolewazo na mabenki yakibiashara ikiwemo utoaji wa mikopo kwa wajasiliamali wadogo wadogo nawale wa kati .

‘’Katika maonesho hayo tunatarajia mgeni rasmi atakuwa naibu waziri wafedha na uchumi Ashatu Kijaji pamoja na mkurugenzi wamifumo ya kibenki kutoka benki kuu ‘’Alisema Leo Nyanduga .

Mwandaaji wa mashindano Nyanduga alisema kuwa katika maonesho hayo yanalenga kukuza uelewa wananchi juu ya taasisi za kifedha ilikuweza kujieletea maendeleo yakiuchumi .

Alisema mwananchi atakayeshiri maonesho hayo ya mabenki hana budi kuwasiliana kupitia barua pepe ya info @bankers.expo.co.tz

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni