Jumatano, 15 Juni 2016

WAZIRI NDALICHAKO AITAKA HELSAB ,NACTE KUZINGATIA VIGEZO VYA UDAILI WA WANAFUNZI NCHINI.

waziri waelimu  nasayansi na Tekinolojia Profesa JOYCE NDALICHAKO




Timothy Marko.
KUFUATIA serikali kuwasimamisha kazi watendaji waliokuwa katika bodi yamikopo (HELSAB) febuari16 mwaka huu kutokana bodi kukiuka taratibu za bodi hiyo,Hatimaye Serikali imebaini dosari mbalimbali  kwenye bodi hiyo nakuweza kuzichukulia hatua .
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Professa Joyce Ndalichako ameitaka bodi yamikopo kuweza kupitia kwa upya dosari zote nakuweza kuzichukulia hatua kwa wahusika walio husika katika dosari hizo.

‘’Serikali inawataka bodi kuwapa mashitaka yakujibu watumishi waliosimamishwa kazi kutokana na udhaifu uliobanikia katika mfumo mzima wa usimamizi wa fedha utoaji naurejeshwaji mikopo ya wanafunzi ‘’Alisema Waziri Joyce Ndalichako .
Waziriwa elimu ,Sayansi na Teknolojia Ndalichako aliwataka bodi hiyo kuweza kurudisha mifumo utoaji mikopo nakuunganishwa nakuweza kuwabaini wanafunzi wanaonufaika mikopo hiyo ambao hawajarudisha mikopo hiyo nakuanza kukatwa ili kurudisha fedha hizo .

Alisema kuwa sambamba nakuwataka bodi hiyo kuweza kufuatilia wanafunzi waliokopa kuweza kurudisha mikopo hiyo,waziri Ndalichako aliitaka bodi hiyo kuweza kuunganisha mifumo yautoaji mikopo unaunganishwa sambamba na ule wa urejeshwaji mikopo hiyo 
.
‘’Serikali imeitaka bodi yamikopo kuweza kutoa ufafanuzi wawanafunzi 168 wachuo kikuu cha Dar es salaam wanaonokekana kukopeshwa shilingi 531,323 ,125 na wanafunzi 919 wa UDOM waliopewa mikopo ya shilingi 2,530,417,440 ambao hawakutambuliwa navyuo hivyo na hakuna ushaidi kuwa fedha zimerejeshwa na bodi yamikopo ‘’Aliongeza Waziri Ndalichako.

Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako ameitaka Bodi na baraza lataifa la elimu yaufundi nchini (NACTE)kuweza kupitia kwa upya sifa za kujiunga vyuo mbalimbali wanavyovisimamia  ikiwemo mitaala yavyuo hivyo .

Aliitaka taasisi hiyo kurekebisha orordha yawatumishi nakuhakikisha wanafanyakazi  wanafanyakazi kulingana na sifa pamoja nataluma staiki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni