Jumatatu, 20 Juni 2016

SERIKALI YA AHIDI KUTOA ELIMU ILI KUPAMBANA NAONGEZEKO LA MIMBA ZA UTOTONI



Timothy Marko.
SERIKALI I imesema kuwa itaendeleza juhudi zake za kutoa elimu yakutosha nakurekebisha sheria yandoa inayoruhusu watoto wenye umri ya miaka 18 kuolewa ili kutokomeza mimba za utotoni na ongezeko la watu nchini .

Akizungumza katika uzinduzi wa Matokeo Muhimu ya utafiti wa afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Mapema hii leo  jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mandeleo Jamii jinsia Wazee na watoto Mpoki Ulisubisya amesema kuwa Serikali itaendelea kutazama kwa upya sheria yamtoto inayoruhusu mtoto kuweza kuolewa akiwa naumri mdogo ilikuondokana natatizo la ongezeko la watu linalotokana nandoa za utotoni .

‘’Kutokana namatokeo yautafiti huu serikali inahidi kuyafanyia kazi matokeo ya utafiti huu ikiwemo kurekebisha sheria zinazo waruhusu watoto walio katika umri mdogo kuweza kuolewa hali inayo changiwa ongezeko la Watu ‘’Alisema Katibu Mkuu Mpoki  Ulisubisya .

Katibu Mkuu Ulisubisya alisema kuwa sambamba nakutokomeza ndoa za utotoni pia serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kutokomeza ugonjwa wa Maralia ,Ugonjwa unasababisha vifo vingi vya watoto nchini .

Hatahivyo Katibu Mkuu huyo aliwataka wananchi kuondokana na tabia kutumia chandarua kwa ajili ya kujikinga naugonjwa wa malaria katika uvuvi wa samaki na badala yake kutumia vyandarua hivyo katika kujikinga na malaria .

‘’kutokana na utafiti huu napenda kutoa wito kwa wananchi kuweza kutumia vyandarua kwa matumizi sahii yakujikinga na Malaria ili kuweza kuondokana navifo vya watoto walipo kati yaumri yamiaka 5 waliokatika hatarikubwa katika maambukizi yam aralia ‘’Aliongeza Katibu Mkuu Mpoki Ulisubisya.

Mkurugenzi wa ofisi ya Takwimu nchini Albina Chuwa amesema kuwa utafiti huo wa afya yauzazi na Mtoto na viashiria vya Maralia nchini wa mwaka 2015 -16 uliweza kufanyika katika maeneo ya Tanzania bara pamoja visiwani kwa kushirikiana na wataalamu wa wizara ya afya ,maendeleo yajamii ,jinsia wazee nawatoto  pamoja nawadau mbalimbali wa maendeleo .
Alisema katika utafiti huo ulilenga kundi lawatu wenye umri wa miaka 15-49  ikiwa nalengo yakujua kiwango cha mambukizi ya vimelea vya maralia naupungufu wa damu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano .

Aidha alisema utafiti wa mwaka 2015 hadi 2016 ulihusisha jumla ya kaya 13,376 zilizochaguliwa kitaaluma kwa njai ya takwimu ili kuweza kuwakilisha kaya zote za Tanzania bara na Tanzania Visiwani.

Alifafanua kuwa viashiria vingi vinapatikana katika ngazi ya taifa,maeneo ay mijini,maeneo ya vijijini pamoja na viashiria vingine vinapatikana katika ngazi ya mikoa.

“tumeweza kutoa taarifa hii mapema yaani miezi mitatu baada ya kumalizika utafiti huu kwa kutumia teknolojia ya kufanya uchambuzi wa wali wa taarifahizi huko kwenye maeneo ya kazi,kwa kutumia kopyuta ndogo”alisema

Aliongeza tafiti zingine zijazo kama hizo zinategemea kutumia tablet moja kwa moja katika mahojiano nah ii itawezesha matokeo kutoka mapema zaidi.

Hatahivyo alitoa shukrani kwa wizara ya afya kutoa ruhusa kwa wauguzi takribani 65 ambao walifanya kazi kubwa na nzito ya kutembelea kaya zote nchini Tanzania ili kukusanya takwimu muhimu za utafiti huo,ambapo walifanya kazi nzuri wanastahili pongezi.
Mwisho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni