Timothy
Marko.
SERIKALI I imesema
kuwa itaendeleza juhudi zake za kutoa elimu yakutosha nakurekebisha sheria
yandoa inayoruhusu watoto wenye umri ya miaka 18 kuolewa ili kutokomeza mimba
za utotoni na ongezeko la watu nchini .
Akizungumza
katika uzinduzi wa Matokeo Muhimu ya utafiti wa afya ya Uzazi na Mtoto na
Malaria Mapema hii leo jijini Dar es
salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mandeleo Jamii jinsia Wazee na watoto Mpoki
Ulisubisya amesema kuwa Serikali itaendelea kutazama kwa upya sheria yamtoto
inayoruhusu mtoto kuweza kuolewa akiwa naumri mdogo ilikuondokana natatizo la
ongezeko la watu linalotokana nandoa za utotoni .
‘’Kutokana
namatokeo yautafiti huu serikali inahidi kuyafanyia kazi matokeo ya utafiti huu
ikiwemo kurekebisha sheria zinazo waruhusu watoto walio katika umri mdogo
kuweza kuolewa hali inayo changiwa ongezeko la Watu ‘’Alisema Katibu Mkuu Mpoki
Ulisubisya .
Katibu Mkuu
Ulisubisya alisema kuwa sambamba nakutokomeza ndoa za utotoni pia serikali
itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kutokomeza
ugonjwa wa Maralia ,Ugonjwa unasababisha vifo vingi vya watoto nchini .
Hatahivyo
Katibu Mkuu huyo aliwataka wananchi kuondokana na tabia kutumia chandarua kwa
ajili ya kujikinga naugonjwa wa malaria katika uvuvi wa samaki na badala yake
kutumia vyandarua hivyo katika kujikinga na malaria .
‘’kutokana
na utafiti huu napenda kutoa wito kwa wananchi kuweza kutumia vyandarua kwa
matumizi sahii yakujikinga na Malaria ili kuweza kuondokana navifo vya watoto
walipo kati yaumri yamiaka 5 waliokatika hatarikubwa katika maambukizi yam
aralia ‘’Aliongeza Katibu Mkuu Mpoki Ulisubisya.
Mkurugenzi
wa ofisi ya Takwimu nchini Albina Chuwa amesema kuwa utafiti huo wa afya
yauzazi na Mtoto na viashiria vya Maralia nchini wa mwaka 2015 -16 uliweza
kufanyika katika maeneo ya Tanzania bara pamoja visiwani kwa kushirikiana na
wataalamu wa wizara ya afya ,maendeleo yajamii ,jinsia wazee nawatoto pamoja nawadau mbalimbali wa maendeleo .
Alisema
katika utafiti huo ulilenga kundi lawatu wenye umri wa miaka 15-49 ikiwa nalengo yakujua kiwango cha mambukizi ya
vimelea vya maralia naupungufu wa damu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano .
Aidha
alisema utafiti wa mwaka 2015 hadi 2016 ulihusisha jumla ya kaya 13,376
zilizochaguliwa kitaaluma kwa njai ya takwimu ili kuweza kuwakilisha kaya zote
za Tanzania bara na Tanzania Visiwani.
Alifafanua
kuwa viashiria vingi vinapatikana katika ngazi ya taifa,maeneo ay mijini,maeneo
ya vijijini pamoja na viashiria vingine vinapatikana katika ngazi ya mikoa.
“tumeweza
kutoa taarifa hii mapema yaani miezi mitatu baada ya kumalizika utafiti huu kwa
kutumia teknolojia ya kufanya uchambuzi wa wali wa taarifahizi huko kwenye maeneo
ya kazi,kwa kutumia kopyuta ndogo”alisema
Aliongeza
tafiti zingine zijazo kama hizo zinategemea kutumia tablet moja kwa moja katika
mahojiano nah ii itawezesha matokeo kutoka mapema zaidi.
Hatahivyo
alitoa shukrani kwa wizara ya afya kutoa ruhusa kwa wauguzi takribani 65 ambao
walifanya kazi kubwa na nzito ya kutembelea kaya zote nchini Tanzania ili
kukusanya takwimu muhimu za utafiti huo,ambapo walifanya kazi nzuri wanastahili
pongezi.
Mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni