Timothy
Marko.
TUME ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) imeridhia kuiazima Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
mitambo yake ili waweze kuchakata
taarifa wakati wa wa zoezi la utoaji wa
vitambulisho hivyo.
Akizungumza
katika kikao kilicho fanyika katika ofisi yatume ya uchaguzi jana jijini Dar es
salaam Mkurugenzi wa tume hiyo Ramadhani Kailima amesema kuwa katika kikao
chake kilichofanyika jana wajumbe wakikao hicho waliweza kukubalianakuhamishwa
kwamitambo hiyo ya NEC kwenda NIDA kwakutumia gharama ya mamlaka hiyo.
‘’Hatua hii
imetokana nakuwepo kwa ugumu wamitambo hiyo kutumiwa na NIDA ikiwa katika ofisi
za NEC Kutokana nakutokuwepo kwa miundombinu yamawasiliano yamkongo wataifa
ambayo imenganisha mahali NIDA wanafanya uchakataji wa vitambulisho ‘’Alisema
Mkurugenzi Wa tume Ramadhani Kailima .
Kailima
alisema kuwa kufuatia kauli ya mwenyekiti watumehiyo Jaji Damiani Lubuva alioitoa
hivi karibuni kwa wajumbe watume yauchaguzi kuwa mitambo hiyo itazimwa na nida
kwa muda wasiku 90 .
Alisema kuwa
tume ya uchaguzi ilinunua mitambo hiyo yatehama kwa jili yakufanikisha zoezi la
wapiga kura na uchaguzimkuu wa mwaka jana.
‘’MITAMBO hii
inauwezo mkubwa wakuchakata taarifa hususan uchakatataji wa alama za vidole ‘’Aliongeza
Kailima .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni