Timothy Marko.
Asilimia 62 yawanawake waliopo katika umri wa kuzaa hufariki dunia kutokana na utoaji wa mimba ambapo kati ya wanawake waliopo kati yaumri 20-30 hupata matatizo ya uzazi yanayotokana nautoaji mimba usiozingatia njia za kitalamu .
Hayo yamesemwa leo na DKAli Saidi mtalamu wa masula ya wanawake Katika Chuo kikuu cha Taifa Muhimbili katika warsha ya siku mbiliya waandishi wa habari iliyoandaliwa na taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya TAWULA ambapo Dr Ali amesema kuwa kati ya wanawake wanaotolewa mimba hufanyiwa na madakitari wasikuwa watalaam hali inayo changia vifo vya wanawake hao.
''Vifo vingi vya wanawake wanaotoa mimba hutokana kufanyiwa huduma hii na watalamu awasio kuwa navigezo na maadili utafiti unaonesha vifo vingi vya wakinamama nawasichana walio kati yamiaka 20-30 hufariki dunia kutokana nakufanyiwa huduma hiyo uchochoroni ''Alisema Dr Ali saidi.
Dk.Ali saidi alisemakuwa huduma yakutoa mimba inahitaji mazingira safi nasalama kwani wengi wao hutoa huduma hiyo katika mazingira ambayosi safi nasalama na vifaa duni hali inayopelekea wanawake wengi kupoteza maisha kutokana kufanyiwa hudumahiyo vichororoni .
Alisema kuwa asilimia 14 ya vifo vya wanawake barani afrika hufariki dunia kutokana navitendo vya utoaji mimba usio kuwa salama ambapo kati yawanawake 1000 wanawake 38 hufariki kutokana na utoaji mimba .
''Katika Mkoa Wa arusha wilayani Hai wanawake 35 walifariki kutokana nakufanyiwa huduma yautoaji mimba kwa kutobolewa kizazi ambapo pia wanawake 155 walifariki kutokana na utoaji wamimba katika hospitali ya muhimbili''Aliongeza Dr Ali Saidi .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni