Timothy Marko.
MAMLAKA ya
mapato nchini (TRA)imewataka wafanyabishara kuzitumia mashine za EFD nakutoa
risiti pindi wanapofanya mauzo za bidhaa zao kwa wateja ilikuiwezesha serikali
kuweza kupata mapato ya tokanayo na kodi .
Akitoa wito
huo mbele ya waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Kamishina mkuu wa taasisi
hiyo Alfayo KIDATA amesema kuwa utekelezaji
wa agizo hilo kwa wafanya biashara linatokana na sheria ya usimamizi wa kodi ya
mwaka 2015 inayomtaka mfanyabishara kutoa risiti za mauzo ya bidhaa anaoyoiuza
.
‘’kwamujibu
wa sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015 ,kutokutoa risiti za EFD nikosa
ambalo adhabu yafaini ama kifungo kisicho pungua miaka mitatu au vyote kwa
pamoja ‘’Alisema Kamishina mkuu wa TRA ALFAYO KIDATA .
Kamishina
mkuu Kidata alisema nivyema wananchi nchini kuweza kujenga utamaduni wa kudai
Risiti mara baada yakufanya manunuzi ilikuweza kutoa ushaidi kuwa mali
iliyonunuliwa imelipiwa kodi serikalini .
Alisema kuwa
hivi karibuni kumekuwa namagari yaliingizwa nchini nakusajiliwa kinyume cha
taratibu za mamlaka hiyo nakusababisha magari hayo yamilikiwe bila kulipiwa
kodi stahiki.
‘’WAMILIKI wa
magarihayo wameshaarifiwa kufika katika ofisi za TRA Ili kufanyiwa uhakiki ili
kuweza kulipa kodi stahiki ‘’Aliongeza Kamishina mkuu ALPHAYO Kidata.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni