Na Magreth Kinabo
Umoja wa Jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo nchini
Tanzania wameandaa kambi ya upimaji wa afya bila malipo kwa watoto wenye umri
chini ya miaka mitano kwa kushirikiana na kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama,mtoto
na vijana ya Mikocheni na Zahanati ya Kiugumo itakayofanyika Machi 13 mwaka huu.
Hayo yalisemwa leo
na Daktari Mstaafu wa Afya ya Jamii na
Familia, Ali Mzige wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
kambi hiyo ya kupima watoto bila malipo.
Dkt. Mzige alisema kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana jumla
ya watoto 289 walipmwa afya zao wenye umri wa chini ya miaka mitano ambapo
alisema asilimia tisa walipatwa maambukizi katika mfumo wa mkojo UTI.
Aliongeza kwamba maambukizi hayo yanachangiwa na uvalishaji wan
epi za watoto maarufu kwa jina la Pampers.
Alisema asilimia saba
walikatawa vimeo, asilimia tano walikutwa na utapia mlo.
Dkt. Mzige alifafanua
kwamba asilimia 20 ya watoto wenye umri katia ya miaka miwili hadi mine walikuwa
na afya duni yya kinywa.
Aliishauri jamii kuwa
na tabia ya kufuata kanuni za afya na kuzingatia lishe bora ili kuweza kuepuka
magonjwa mbalimbali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni