DSE YASHUKA
Timothy Marko.
Mauzo yahisa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE)
yamepungua kutokana na baadhi ya
wafanyabishara wanaonunua hisa katika soko hilo kuhifadhi fedha zao kwajili ya
msimu wa sikukuu ya pasaka .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Afisa
Mwandamizi wa masoko katika soko la hisa jijini Dar es salam MARY KINABO alisema
mauzo yameshuka kutokana na akaunt ya TBL kushuka katika wiki iliyopita.
“Mauzo katika wiki ya hisa yameshuka kutoka bilioni
7.8 hadi bilioni 7.2 huku kampuni zilizoongoza kwa mauzo ni pamoja na TBL, DCB,
NMB, ACCASIA, pamoja na East Africa Brueweries ,” alisema Kinabo.
Aidha Kinabo alisema kuwa secta ya viwanda imeshuka
kwa kwa asilimia 10
Pia alitoa wito kwa wanafunzi wa elimu ya juu
kuendelea kujisajili katika shindano la Schollar investment challenge ili
kuweza kukuza hali yao ya kiuchumi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni