Alhamisi, 25 Februari 2016

WAZIRI MKUU AWATAKA MAWAZIRI KUZINGA TIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA


Tokeo la picha la picha za waziri mkuu majaliwa

Na Anitha Jonas
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewaasa Mawaziri na Manaibu Waziri kuzingatia sheria ya Maadili kwa Viongozi wa Utumishi wa Umma kwani maadili ni nyenzo  kubwa katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.

Mheshimi wa Majaliwa ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua semina ya Maadili kwa Mawaziri na Manaibu Waziri inayolenga kuwajengea uwezo mkubwa yanamna kiongozi wa utumishi wa umma anavyotakiwa kutekeleza majukumu yake bila kukiuka maadili.

“Chimbuko la Maadili ya Utumishi wa Umma ulianza tangu siku nyingi na umekuwa ukitajwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo katika Katiba ya nchi ya mwaka 1977, Sheria za Utumishi wa Umma pamoja na Kanuni za Utumishiwa Umma,”alisemaMajaliwa.

Akiendelea kuzungumza katika Semina hiyo WaziriMkuu alisisitiza kuwa Semina hiyo siyo semina elekezi kwa viongozi hao kama jinsi imekuwa ikijadiliwa katika mitandao ya kijamii, bali ni semina inayolenga kutoa mwongozo wa maadili ya viongozi wa umma na utekelezaji wa Hati ya Ahadi ya Uadilifu na mada katika semina hiyo zitahusu masuala ya maadili tuu.

Kwa upande wa Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda kutoka Ofisi ya Rais Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma amesema semina ya maaadili kwa viongozi ni jukumu la Sekretariati ya maadili kuandaa kwani hiyo ni sehemu ya majukumu ya Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma na wao ndiyo wenye wajibu wakuhakikisha viongozi wa utumishi wa umma wanazingatia maadili.

“Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Utumishi wa Umma inamamlaka ya kufanya uchunguzi kwa kiongozi yoyote wa umma atakayesikika kukiuka maadili kama kiapo cha ahadi za uadilifu kinavyosema,”alisema Jaji Mstaafu Salome.

Aidha Kamishna wa Maadili huyo aliendelea kusema Ofisi ya Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya rasimali fedha ambapo wanazaidi ya miaka mitatu wameshindwa kufanya uhakiki wa mali za viongozi pamoja na uchunguzi kutokana na changamoto hiyo.

Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na Shirika la USAID.


Waziri Mkuu awataka Mawazi kuzingatia Maadili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni