Alhamisi, 25 Februari 2016

TAASISI YA TWAWEZA YATOA MAONI YA UTAFITI YA UCHANGIAJI WA SEKTA YA ELIMU NCHINI

Tokeo la picha la logo ya twaweza
 Timothy Marko.
Taasisi ya utafit ya TWAWEZA  imetoa utafiti wake kuhusiana na Agizo la  Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli yakutaka elimu  bure kuanzia elimu ya msingi hadisekondari ambapo imesema kuwa zaidi ya asilimia 88 yawananchi wanaamini kuwa ahadi hiyo itatekelezwa .

Akisomamatokeo ya utafiti huo jijini Dar es salaam  Profesa Kitila Mkumboamesema kuwa katika utafiti huo uliofanywa katika mikoa mbalimbali yaTanzania bara na Zanzibar ambapo jumla ya watu 1,894 waliweza kuhojiwa katika utafiti huo,aslmia 89wakiri kulipa michango mashuleni kati yao asilmia 80 walilipa zaidi shilingi100,000 kwamwaka wakatiasilmia 80 walilipa shilingi 50,000kwa mwaka kama michango yashule

Profesa kitila alisema kwamujibu wa utafiti huo uloneshakuwa wazazi huchangia michango ya ulinzi kwa kiasikikubwa ikifuatiwa namichango ya madawati wakati huo huo utafiti ulibainisha kuwa ruzuku inayotolewa naserikali katika shulembalimbali haitoshelezi .

‘’Ruzuku inayotolewa huelekezwa kwenye vitabu na nyenzo mbalmbali za kujifunzia niaslimia 40 wakati huo huo vifaa vya kuandikia vikishika asilimia 20,hivyo shule zinapaswa kuwa makini nakiwango  kidogo cha fedha kinachopatikana kwani vituvingi ambavyo wazazi huchangiahavijumuishwa kwenye ruzuku ‘’Alisema Profesa kitila Mkumbo.


Nao watalaam na wadau wa mambo  ya elimu kutoka ndani na nje ya nchi wamesema  serikali ya awamu ya tano nibora sasa ikaweka nguvu kubwa katika kusaidia chakula mashuleni  ili kuongeza uelewa wa wanafunzi ,amakuwashirikisha wazazi kata kucha ngia chakula  kuliko kuiachia serikari mzigo mkubwa wakuhudumia kilakitu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni