Timothy Marko.
WANAFUNZI wa
vyuo vikuu nchini wametakiwa kukuza uelewa wa shughuli za soko lahisa la Dar es
salaam(DSE ) ili kuweza kupata fursa ya ajira ili kuondokana na umasikini.
Wito huo
umetolewa na Meneja Mauzo wa soko la hisa la Dar es salaam Patrick Mususa
wakati akizungungumza na waandishi wa Habari jijini kuhusiana na shindano la Scholar
Investment Challenge linalotarajiwa
kuanza Mwezi March Mwaka huu .
‘’ifikapo
Mwezi ujao tunatarajia kuanziasha shindano letu lijulikanalo kama Scholar
Investment Challenge shindano hili tuna tarajia kulianzisha mwezi March hadi
juni mwaka huu’’ Alisema Meneja Mauzo na Biashara Patrick Mususa .
Meneja
Mususa alisema kuwa shindano hilo litajumuhisha wanafunzi wa vyuo vikuu
vilivyosajiliwa na tume ya vyuo vikuu nchini (TCU)ambapo shindano hilo
litafanyika kwa washiriki hao kupitia simu za mikononi .
Alisema kuwa
Taasisi hiyo inatarajia kuongeza mifumo
mbali mbali ya utowaji wataarifa kwa wateja wake ikiwemo kuboresha mifumo hiyo katika simu za
viganjani zenye uwezo wa mifumo ya Internet.
‘’Tunatarajia
kuboresha huduma zetu za uuzwaji wa hisa na utowaji wataarifa za mwenendo wa
soko la mitaji kupitia simu za viganjani
‘’Aliongeza Mususa .
Mususa
aliongeza kuwa katika shindano hilo washindi wataweza kuajiliwa katika taasisi za kibenki .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni