Jumatatu, 25 Januari 2016

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NCHINI WAASWA KUJIUNGA NASOKO LAHISA ILI KUONDOKANA NATATIZO LA AJIRA.



Timothy Marko.
WANAFUNZI wa vyuo vikuu nchini wametakiwa kukuza uelewa wa shughuli za soko lahisa la Dar es salaam(DSE ) ili kuweza kupata fursa ya ajira ili kuondokana  na umasikini. 

Wito huo umetolewa na Meneja Mauzo wa soko la hisa la Dar es salaam Patrick Mususa wakati akizungungumza na waandishi wa Habari jijini   kuhusiana na shindano la Scholar Investment  Challenge linalotarajiwa kuanza Mwezi March Mwaka huu .

‘’ifikapo Mwezi ujao tunatarajia kuanziasha shindano letu lijulikanalo kama Scholar Investment Challenge shindano hili tuna tarajia kulianzisha mwezi March hadi juni mwaka huu’’ Alisema Meneja Mauzo na Biashara Patrick Mususa .

Meneja Mususa alisema kuwa shindano hilo litajumuhisha wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyosajiliwa na tume ya vyuo vikuu nchini (TCU)ambapo shindano hilo litafanyika kwa washiriki hao kupitia simu za mikononi .

Alisema kuwa Taasisi hiyo inatarajia kuongeza mifumo  mbali mbali ya utowaji wataarifa kwa wateja wake  ikiwemo kuboresha mifumo hiyo katika simu za viganjani zenye uwezo wa mifumo ya Internet.

‘’Tunatarajia kuboresha huduma zetu za uuzwaji wa hisa na utowaji wataarifa za mwenendo wa soko la mitaji kupitia  simu za viganjani ‘’Aliongeza  Mususa .
Mususa aliongeza kuwa katika shindano hilo washindi wataweza  kuajiliwa katika taasisi za kibenki .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni