Jumapili, 17 Januari 2016

SEKTA YAKIBENKI YAIMARISHA KIWANGO CHA MAUZO YA HISA DSE



Na Timothy Marko.

KIWANGO cha mauzo yahisa kimeweza kupanda hadi kufikia shilingibilioni  6.7 kutoka shilingi bilioni 4 ambapo ongezeko hilo nisawa na asilimia 50 kwa wiki iliyopita .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini mapema hii leo, Meneja mauzo na biashara  wa soko la hisa la Dar es salaam DSE, Partick Mususa amesema kuwa ongezeko hilo limetokana nakuongezeka kwa kiwango cha hisa zilizoweza kuuzwa sokoni hapo ambapo  jumla hisa bilioni 12zilingia kwenye mauzo  ikilinganishwa hisa bilioni 3.6 zilizouzwa kwa kipindi cha wiki moja iliyo pita .

‘’Makapuni yaliongoza katika uuzwaji wa hisa zake kupitia soko la hisa la Dar es salaam DSE nipamoja na benki ya CRDB,TBL SIMBA Cement ‘’Alisema Patrick Mu susa.

Meneja Mauzo na Biashara Patrick Mususa amesema kuwa kiwango cha mauzo hayo yahisa kuongezeka kutokana na hududuma yasekta yakibenki kuweza kuimarika hali inayo changia kuimarika kwa idadi yamauzo yahisa katika soko hilo .

Alisema kuwa sambamba na kuimarika kwa sekta yakibenki nchini sekta ya viwanda imeweza kushuka kutkana sekta hiyo kutegemea sekta nyingine ilikuweza kukua .

‘’Sekta ya viwanda imeza kushuka kutokana kuwategemezi kwa sekta nyingine ilikuweza kukukuza uchumi nakuweza kuimarisha soko la mtaji katika soko ‘’Aliongeza Mumsusa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni