Timothy Marko.
MKURUGENZI
wa taasisi ya haki elimu nchini Jonh Kalage ameitaka serikali kuratibu sera ya
elimu nchini kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ilikuweza kukuza
ushindani wa wahitimu katika soko la ajira .
Akizungumza
katika kongamano la kuratibu nakuchambua ripoti ya marekebisho yasera yaelimu
nchini, Jonh Kalage amesema kuwa sekta ya teknolojia na sayansi imekuwa ikikua
kwa kasi hali inayochangia sekta ya elimu nchini kubaki nyuma kutokana
nakutoendana nasoko la ajira linalowahitaji rasmali watu ambao wanaendana na
mabadiliko ya sekta hiyo .
‘’Mabadiliko
yasayansi na teknolojia yanakuwa kwa kasi ambapo sekta ya elimu inatakiwa
kuendana na kasi hiyo ya mabadiliko ya sayansi ili tuweze kuwa narasimali watu
wenye ubora nakuleta ushindani katika soko la ajira ‘’Alisema Mkurugunzi Jonh
Kalage .
Mkurugenzi
Kalage alisema kuwa ili elimu iwebora nilazima iendane na ubora na uwezo wa
wahitimu katika kuweza kuzikabili changamoto mbalimbali na utatuzi wa masuala
ya nayomkabili mhitimu huyo katika mwenendomzima wa maisha .
Alisema kuwa
sambamba na mhitimu kuwa nauwezo wakuzikabili changamoto hizo pia lugha yakufundishia iwe rahisi ili
kumuwezesha muhitimu huyo kuchambua nakuyaelewa mambo kwa kina tofauti
ilivyokuwa hivi sasa ambapo kunalugha mbili zinazo tumika.
‘’Sera hii
haichambua na kubainisha uchaguzi wa lugha yakufundishia tuna ishauri serikali
kuweza kutathimini lugha ya kufundishia ilikuwepo na usawa katika utoaji wa
elimu katika ngazi zote ‘’Aliongeza Kalage .
Muhadhiri namchambuzi wa masuala yaelimu nchini Suleman
Samra amesema kuwa lazima mfumo wa elimu
uendane na mafunzo ya ufundi ambayo
utamuwezesha muhitimu kuwa na uwezo na ujuzi .
Alisema kuwa
lazima elimu inayotolewa iwenauwezo wakubadilisha mtu kifikra na kitabia na
uwezo kuwasiliana na kuwa naujuzi wa kutatua matatizo .
‘’Mfumo
waelimu nilazima uwe namisingi ifuatayo ikiwemo ujuzi utakao mbadilisha mtu
kitabia kiujuzi kumjenga naujuzi wa
ufundistadi na utatuzi wa changamoto ‘’Aliongeza
Samra .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni