Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatano, 23 Desemba 2015
WAZIRI KITWANGA AWAIGIZA IDARA YA UHAMIAJI KUPITIA VIBALI VYA WAGENI WANAOISHI NCHINI KINYUME NA SHERIA .
Timothy Marko .
KATIKA kuhakikisha tatizo la wahamiaji Haramu linakomeshwa nchini, waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga ameiagiza idara ya uhamiaji kuweza kupitia vibali vya wageni wanaofanya kazi hapa nchini nakuweza kutoa ripoti za taarifa zavibali vya wageni hao ifikapo jumatatu ijayo .
Agizo hilo limekuja kutokana na kuwepo kwa malamiko ya utoaji wa vibali vya wagenikwajili yakufanyakazi hapa nchini nakuwa vibali hivyo vimekuwa vikitolewa kwa mianya ya rushwa nakusababisha baadhi ya wananchi kukosa ajira .
Akizungumza katika kikao kilicho wa kutanisha maofisa wa uhamiaji katika idara hiyo mapema hii leo jijini Dar es salaam Waziri CHARLES KITWANGA alisema kuwa nilazima taasisi hiyo ijiimarishe katika utendaji wake na kuhakikisha watumia mtandao wakomputa kuwawezesha wananchi na wageni kuweza kujaza fomu za vibali vyakukaa nchini na kuondoka nchini ili kuepusha msongamano wawatu wanaomba vibali kutoka kwenye idara hiyo .
‘’Ninaiagiza idara hii ya uhamiaji iweze kupunguza muda wa utoaji wa pasipoti ambapo ninataka paspoti itolewe kwakipindi cha siku tatu ,naparmite itolewe baada yasiku tano ‘’Alisema Waziri Kitwanga .
WAZIRI KITWANGA alisema kuwa kasumba ya utoaji wavibali vyakuishi nchini pamoja naajira katika idara hiyo kwa minadi ya rushwa lazima vitendo hivyo vikomeshwe nakuwataka wakuu waidara hiyo kukomesha vitendo vya rushwa .
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni