Ijumaa, 18 Desemba 2015

SERIKALI YAWATAKA MFUKO WA PESHENI PSPF KUAKAMILISHA MALIPO YA WASTAAFU.

Timothy Marko. SERIKALI imetaka mfuko wapesheni kukamilisha malipo yafedha ya shilingi bilioni 177 ambazo zimetolewa naserikali kupitia taasisi hiyo yaumma kwa ajili yakuwalipa wataafu kuanzia mwezi April hadi Novemba mwaka huu . Akizungumza katika ziara yakushitukiza aliyoifanya mapema hii leo katika makao makuu ya ofisi hizo zilizopo katikati ya jiji la Dar es salaam Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr.AShatu Kijaji amesema kuwa SERIKALI inataka taasisi hiyo ikakamilisha malipo yafedha hizo kwa wastaafu ambazo zimebakia ndani yakipindi chasiku saba . ‘’SERIKALI inaipa mfuko wa pesheni wa umma wa PSPF Kukamilisha madai ya malimbikizo yamafao kwa staafu kwakipindi cha siku saba fedha hizo ziwe zimekamilika ‘’Alisema Naibu waziri Ashatu Kijaji . Naibu waziri ASHATU kijaji alisema kuwa jumla ya shilingi bilioni 177 zimekuwa zikidaiwa nawastaafu waliojiunga namfuko huo wa hifadhi kwa jamii wa PSPF lakini hadi kufikia Novemba mwaka huu jumla shilingi bilioni 174 zimeshalipwa nakuwa jumla shilingi bilioni 70 bado hazikuweza kufikia wastaafu hao . KATIKA hatua nyingine Mkurugenzi mkuu wa PSPF Adamu Mayingu amesema kuwa taasisi hiyo haja wahi kupokea michango ya wastaafu kwakipindi cha miezi saba . Adamu Mayingu amesema kuwa awali ipata jumla ya fedha bilioni 35 ambazo zilitumwa kwa wakuu wa mashirika hayo yauma lakini jumla bilioni 35 bado hazikukulipwa na mashirika hayo . ‘’Tutaendelea kuzifuatilia hizo fedha bilioni 35 zilizobakia kama naibu waziri alivyo elekeza ambapo jumla fedhabilioni 70 zilitumwa kulipwa kwa staafu hao kwanijia yahudi ambapo jumla ya hundi 444 zimeshatoka ‘’Alisema Mayingu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni