Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatatu, 7 Desemba 2015
KIWANGO CHA UNUNUZI WA HISADSE CHA FIKIA SHILINGI BILIONI 65
Timothy Marko.
KIWANGO cha mauzo ya hisa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE)kimeongezeka kutoka shilingi bilioni 34kwa wiki iliyopita hadi kufikia bilioni 65 ambapo aongezeko hilo nisawa na asilimia 65 hali iliyoime changiwa na kuongezeka kwa kiwango cha makampuni yaliyo orodheshwa katika soko hilo la hisa .
Akizungumza na waandishi wa habarimapema hii leo jijini Dar es salaam, Meneja mauzo na biashara Patrick Mususa amesema kuwa ongezeko hilo lina endana sambamba nakukua kwa idadi ya makampuni yaliyo orodheshwa katika uuzwaji wa hisa kutoka makampuni ishirini nakufikia makampuni ishirini na moja kwa kipindi cha wiki iliyopita .
‘’Hali ya soko katika uuzwaji wa hisa imeongezeka kutoka makampuni ishirini nakufikia makampuni ishirinina moja wakati huo huo sekta ya viwanda imeweza kukukua nakufikia asilimia arobaini namoja na sekta ya kibenki imeweza kupungua ‘’Alisema Meneja Biashara na Mauzo Patrick Mmsusa .
Meneja Biashara Msusa alisema kuwa sekta ya kibiashara imeweza kukukua hali iliyochangiwa na kampuni ya SWISPORT kuuza hisa zake kupitia soko la mitaji kutoka soko la hisa la Dar es salaam na wakati huo huo baadhi ya wanahisa kuweza kununua hisa zao katika soko hilo la mitaji kwa kupiga namba *150*36# .
Alisema kuwa kiwango cha hati fungani kimezidi kuboreka Zaidi baada ya benki ya EXIM kuboresha uuzwaji wa hati fungani Tangu Novemba 13 mwaka huu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni