Ijumaa, 4 Desemba 2015

ADB YAIPATIA TANZANIA BILIONI 585 .25 KUBORESHA SEKTA YA MIUNDOMBINU

Timothy Marko. Jumla ya shilingi bilioni 585.25 zina tarajiwa kuwekezwakatika sekta ya miundombinu ikiwa ni hatua ya serikali ya Tanzania na benki ya maendeleo ya afrika (ADB) kuboresha sekta ya miundombinu katikamikoa ya nyanda za juu kusini pamoja na mikoa ya pwani na Tanzania visiwani . Akitia saini katika mkutano wa makubaliano hayo jijini Dar es salaam mapema hii leo,katibu Mkuu wa wizara ya fedha SERVANUS Likwelile amesema kuwa fedha hizo zinatarajiwa kukamilisha ujenzi wa miradi ya barabara katika mikoa ya Tabora koga mpanda yenye urefu wa kilometa 342 ,pamoja na barabara zilizopo vijijini Zanzibar yenye urefu wa kilometa 20 ,mbiga –mbamba bay (kilometa67 ),BUBUBU Mahonda –Mkokotoni kilometa 31. ‘’Tunapenda kuishukuru Benki ya maendeleo ya afrika kuweza kuisadia SERIKALI ya Tanzania katika kuboresha sekta ya miundombinu kwa kuipatia kiasi shilingi bilioni 585 .25 ikiwa nijitiahada za benki hii katika kusaidia sekta mbalimbali za uchumi ‘’Alisema KATIBU MKUU Servenus Likwelile . Servenus Likwalile alisema kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na benki hiyo ya maendeleo katika kuboresha miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya bara bara . Aidha ,Muwakilishi mkaazi wa Benki ya maendeleo ya afrika ADB Tonia Kandierio amesema kuwa miradi hiyo ya barabara inalengo ya kuimarisha miundombinu TANAZANIA bara pamoja na visiwani ilikuweza kupunguza msongamano katika bara bara nakuimarisha sekta ya miundo mbinu . Muwakilishi Mkazi wa ADB Kandiro alisema kuwa miradi mbali mbali ya bara bara inatarajiwa kamilishwa katika mikoa Zanzibar ,Mpanda pamoja bubu Mahonda . ‘’Hii miradi ya ,maendeleo inalenga kukuza miradi yamaendeleo nakukuza uchumi nakuondokana naumasikinini kwakuimarisha miradi mbali mbali ya maendeleo ‘’Alisema Kandiro.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni