Jumatano, 30 Desemba 2015

BARAZA LA TAIFA LA UJENZI LAPOKEA MALALAMIKO 41



Timothy Marko.

BARAZA la Taifa la ujenzi nchini limesema kuwa limepokea Malalamiko  41 Katika halimashauri mbalimbali ambapo kati ya hayo saba yapo  katika ngazi za halimamashauri hizo zikisubiri Maamuzi ya baraza hilo.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, AfisaMtendaji mkuu  wa baraza hilo, Mhandisi Leonard Chamuriho, alisema kuwa katika kutatua migogoro hiyo ya ujenzi nchini Baraza hilo limeweza kuwajengea uwezo watalaam wandani ilikuleta usuluhishi wa migogoro hiyo.



‘’Katika kutatua migogoro hii tunashirikiana na mipango miji kwa kuwa shirikisha wadau wakiwemo wenye mali pamoja na makandarasi lakini kati ya migorogoro hiyo bado ipo katika hatua za awali katika ngazi ya utatuzi’’Alisema  Chamuriho.



Chamuriho alisema kuwa katika sekta hiyo yaujenzi imekuwa ikikabiliwa na tatizo la ujenzi holela ambao haukidhi viwango vya mipango miji hali inayopelekea  badhi yamiradi kutokidhi viwango hivyo  .



 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni