BARAZA LA TAIFA LA UJENZI LAPOKEA MALALAMIKO 41
Timothy Marko.
BARAZA la
Taifa la ujenzi nchini limesema kuwa limepokea Malalamiko 41 Katika halimashauri mbalimbali ambapo kati
ya hayo saba yapo katika ngazi za
halimamashauri hizo zikisubiri Maamuzi ya baraza hilo.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam, AfisaMtendaji mkuu wa baraza hilo, Mhandisi Leonard Chamuriho, alisema
kuwa katika kutatua migogoro hiyo ya ujenzi nchini Baraza hilo limeweza
kuwajengea uwezo watalaam wandani ilikuleta usuluhishi wa migogoro hiyo.
‘’Katika
kutatua migogoro hii tunashirikiana na mipango miji kwa kuwa shirikisha wadau
wakiwemo wenye mali pamoja na makandarasi lakini kati ya migorogoro hiyo bado
ipo katika hatua za awali katika ngazi ya utatuzi’’Alisema Chamuriho.
Chamuriho
alisema kuwa katika sekta hiyo yaujenzi imekuwa ikikabiliwa na tatizo la ujenzi
holela ambao haukidhi viwango vya mipango miji hali inayopelekea badhi yamiradi kutokidhi viwango hivyo .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni