Alhamisi, 10 Septemba 2015

MEMBE AWATAKA WAANGALIZI WAKIMATAIFA WA UCHAGUZI KUTOJIHUSISHA NA MASUALA YA KISIASA .

Timothy Marko . WAANGALIZI wapatao 600 kutoka ndani nanje ya nchi ,wanatarajia kusimamia uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika October 25 mwaka huu ambapo wangalizi hao wametakiwa kusimamia uchaguzi huo pasipo kuwa na misimamo yakisiasa ili kufanyikisha uchaguzi huru na wa haki .
Akizungumza katika mkutano uliowajumuisha mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini jijini Dar es salaam mapema hii leo,waziri wa mambo ya nje Benard Membe amesema kuwa kati yahao 400 wameshawasili ilikusimamia uchaguzi huo .
''WAANGALIZI wapatao 600 wanatarajia kusimamia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika october 25mwaka huu ambapo kati 400 tayari wa mekwisha kutibitisha kushiriki kusimamia uchaguzi huo ''Alisema Benard Membe .
Waziri Membe aliwataka wangalizi hao kutojihusisha na masuala ya Kisiasa ikiwemo kuwasaidia wagombea wanao wania kiti cha urais kushinda uchaguzi huo,nakusitiza haki itendeke kwa wagombea wote nakutokuwa na upendeleo kwa wagombea .
Alisema kuwa Baadhi ya wangalizi wanaotarajiwa kusimamia uchaguzi huo wanatoka nchi za jumuhia ya ulaya ,Marekani ,pamoja nanchi zajumuhia zakusini mwa afrika SADEC.
''Wangalizi wote wauchaguzi mkuu nilazima wajaze fomu ilikuweza kupata uthibitisho na kuzirejesha fomu hizo kwa wakati ,pia wangalizi hawa hatutarajii kuzungumza na waandishi wa habari ''Aliongeza waziri Membe .
MEMBE aliongeza kuwa Taarifa zihusuzo mwenendo wauchaguzi mkuu zitatolewa baada ya uchaguzi mkuu kufanyika nakumalizika ,nakusisitiza kuwa serikali haitaficha kitu chochote kihusuyo mchakato huo na baadhi yameneo yakambi zajeshi yatazuliwa kuingia ilikuweza kufuatilia mchakato huo .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni