Timothy Marko.
KUFUATIA chama cha demokrasia na maendeleo nchini(CHADEMA)Kutangaza kuwa inatarajia kufanya mkutano wa Hadhara Agosti 22 mwaka huu katika uwanja wa taifa uliopo jijini Dar es salaam Serikali imepiga marufuku juu ya chama hicho kutumia uwanja huo katika harakati za kisiasa za chama hicho .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salam mapema hii leo Mkurugenzi wa idara Habari Maelezo ASAH Mwambene amesema kuwa hatua ya kupiga marufuku kwa wanasiasa kutumia uwanja huo imetokana na chama cha chadema kuomba uwanja huo ilikusudi kumtambulisha mgombea wao wakiti cha Urais Edward LOWASA ili aweze kupata ridhaa ya kuwaongoza wananchi kupitia chama chake ifikapo Oktoba 25 mwaka huu .
''SERIKALI imeona kuwa uwanja wataifa usitumike kisiasa kwani utasa sababisha mihemuko yakisiasa hususa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi ''Alisema Mwambene.
Mwambene alisema hatua hii yakuvipiga marufuku vyama vyasiasa kufanyia mkutano katika uwanja wataifa si kwa chama cha demokrasia namaendeleo tu bali nikwa vyama vyote vyasiasa .
Alisema Nawaomba jamani wanasiasa tusiutumie wanja wa taifa kwa shughuli za kisiasa kwani uwanja huu haukujengwa kwa minadi ya kisiasa bali kwaminadi ya kimichezo hivyo basi nawaomba tu uwache uwanja huu tusije tukaleta machafuko yakisiasa .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni