Timothy Marko
Serikali imesema
Tayari imeshaanza kufanya uratibu wa ajira za nje ya nchi ikuepukana migogoro
itokanayo na baadhi ya watanzania kufanyishwa kazi zisizo nastaaha na kunya nya
swa na baadhi ya waajiri walipo katika nchi za nje .
Akizungumza
nawaandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Afisa habari wa Taesa
Jamila Mbaruku amesema kuwa serikali imeanza kupitia mikataba ya ajira za nje
ya nchi kabla ya watanzania wanaotarajia kufanya kazi nje ya nchi .
‘’Tunao
utaratibu wa kuhakiki mikataba yaajira mkataba huu wa siku 14 unalenga
kujiridhisha kwa muajiriwa anayekwenda kufanya kazi katika nchi husika ‘’Alisema
Jamila Mbaruku .
Mbaruku
alisema kuwa katika mkataba huo unavyo vipengele vya lugha ya kingereza
nakiswahili ilkuweza kumuwezesha muajiriwa kuweza kufahamu makubaliano na
majukumu ya kazi katika kampuni anayokwenda
kufanyia kazi .
Alisema kuwa
endapo kutakuwa navitendo vya unyanyasaji wa kijinsia au kingono katika
sehemuanazofanyia kazi mtanzania huyo katika nchi husika muhanga wa tukio hilo
anaweza kuripoti katika ubalozi wa Tanzania katika nchi husika ili wakala
waajira nchini Tanazania aweze kusitisha ajira hiyo .
‘’wakala
wajira anatakiwa kuuwasiliana naubalozi ilkuweza kumrudisha Mhanga huyo nchini
mwake ,namashariti ya mkataba wake lazima upitiwe wakala wajira ‘’aliongeza
Jamila Mbaruku.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni