Jumatatu, 20 Aprili 2015

SERIKALI :TUMEANZA KUPITIA MIKATABA YA AJIRA NCHI ZA NJE

Timothy Marko
Serikali imesema Tayari imeshaanza kufanya uratibu wa ajira za nje ya nchi ikuepukana migogoro itokanayo na baadhi ya watanzania kufanyishwa kazi zisizo nastaaha na kunya nya swa na baadhi ya waajiri walipo katika nchi za nje .
Akizungumza nawaandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Afisa habari wa Taesa Jamila Mbaruku amesema kuwa serikali imeanza kupitia mikataba ya ajira za nje ya nchi kabla ya watanzania wanaotarajia kufanya kazi nje ya nchi .
‘’Tunao utaratibu wa kuhakiki mikataba yaajira mkataba huu wa siku 14 unalenga kujiridhisha kwa muajiriwa anayekwenda kufanya kazi katika nchi husika ‘’Alisema Jamila Mbaruku .
Mbaruku alisema kuwa katika mkataba huo unavyo vipengele vya lugha ya kingereza nakiswahili ilkuweza kumuwezesha muajiriwa kuweza kufahamu makubaliano na majukumu ya kazi katika kampuni anayokwenda  kufanyia kazi .
Alisema kuwa endapo kutakuwa navitendo vya unyanyasaji wa kijinsia au kingono katika sehemuanazofanyia kazi mtanzania huyo katika nchi husika muhanga wa tukio hilo anaweza kuripoti katika ubalozi wa Tanzania katika nchi husika ili wakala waajira nchini Tanazania aweze kusitisha ajira hiyo .
‘’wakala wajira anatakiwa kuuwasiliana naubalozi ilkuweza kumrudisha Mhanga huyo nchini mwake ,namashariti ya mkataba wake lazima upitiwe wakala wajira ‘’aliongeza Jamila Mbaruku.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni