Timothy Marko.
Jeshi
lapolisi kanda maalum jijini Dar es salaam limesema kuwa limeimarisha doria
katika maeneo ya jiji la Dar es salaam ilkuweza kukabiliana navitendo vya
kihalifu vinavyotokea katika mwisho wa mwaka nakuwa toa wasiwasi wananchi
kuhusiana hali yausalama katika jiji hilo .
Akizungumza
na waandishi wahabari mapema hii leo jijini Dar es salaam, Kamishina SULEMANI
KOVA amesemakuwa katika kipindi hiki chamwisho wamwaka kunakuwa na matukio
mengi yakuhalifu ya uporaji fedha naujambazi wakutumia silaha hivyo jeshi hilo
limeanza operesheni maalumu ya kuzuia vitendo vyakiahalifu kuanzia leo usiku
ilikukabiliana navitendo vya uhalifu hususan mwisho wamwaka .
‘’Kama
inavyofahamika kuwa hiki nikipindi cha mwisho wa mwaka watu wengi hukusanya
fedha kwajili ya mahitaji yao hususan kuwaandalia watoto ada za shule nakufanya mipango mbalimbali katika
mwisho wamwaka wengi wao huendalikizo
katika kipindi hiki pia katika kipindi hiki uhalifu hukua kwa kiwango
chajuu sana hivyo sisi kama jeshi lapolisi tumeanzisha operesheni maalum ya
kupambana na uhalifu ‘’Alisema Suleiman KOVA.
Kamanda Suleiman
kova amesema kuwa kutokana na hali ya uhalifu kuongezeka katika kipindi cha
mwisho wamwaka nawahalifu hao kutaka njia za mkato za kujikimu kimaisha jeshi
hilo halitokaa kimya kuona vitendo hivyo vikiendelea na mali za wananchi
kupotea hivyo jeshi hilo lita anza opesheni hiyo kuanzia usiku wa hileo
ilikukabiliana na vitendo hivyo.
Amesema kuwa
opesheni hiyo itajumuhisha msako wa wahalifu mtaa kwa mtaa katika maeneo yote
ya jiji la Dar es salaam na kuwa taka wananchi kusosafirisha fedha bila kuwa na
escott yapolisi kwani eskot hiyo nibure.
‘’Kitendo
cha wananchi wanao safirisha fedha bila kuwa na escott ya polisi ikiwemo
kusafirishafedha katikabuti za gari hiyo nisawa na kujitafutia kifo hivyo
nawaomba wananchi wanaosafirisha fedha kuomba escot yapolisi ilkuepukana hatari
yakupoteza maisha yao ‘’Aliongeza Kamanda Suleiman kova.
Katika
hatuanyingine jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa waujambazi 13 kwatuhuma
zakupora fedha katika benki ya stanbic iliopo jijini Dar es salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni