Timothy Marko.
KUFUATIA
jeshi la polisi nchini Kudaiwa kuwapiga waandishi wa habari wakiwa katika
majukumu yao katika kufuatilia mahojiano maalum na MWENYIKITI wa chama cha Demkrasia
na maendeleo(CHADEMA) FREEMAN MBOWE,
JUKWAA la wahariri nchini limeitaka jeshi hilo kujinasua katika tuhuma
nzito kwa kuwaondosha maafisa wake wanaotuhumiwa kuwapiga waandishi.
Akizungumza
na waandshi wa habari mapema hii leo, Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini
TEF Absalom kibanda amesemakuwa kutokana najeshi hilo kuwa kimya imeonesha wazi
walihusika natukio hilo la kuwa shambulia waandishi wa habari katika tukio
lililofanyika jana .
‘’Jeshi
lapolisi linapaswa kufanya kile kilicho fanywa napolisi wenzao wa Brazill julai
mwaka huu ambako askari polisi wanne
walionaswa katika mikanda ya video wakiwashambulia waandishi wa habari
walisimamishwa kazi ilikupisha uchunguzi dhidi yao ‘’Alisema Absalom kibanda
Kibanda
alisemakuwa wataendelea kutumia kalamu zao na zananyingine za kikazi kulaani
matukio hayo aliliyofanywa najeshi hilo kwakuwashambulia waandishi wa habari
pamoja na athari zake kwa umma ili umma utoe hukumu inayostahili kwa jeshi
hilo.
Alisema kuwa
serikali inapaswa kuchunguza kwakina matukio hayo ya jeshi lapolis kuwa
shambulia waandishi wa habari ilikujua hasira za polisi dhidi ya waandishi zina
tokana na nini wanataka kuficha nini watathimini athari zake katika mfumo mzima
wautoaji na upatikanaji wa habari nchini .
‘’jukwaa
linaamini kuwa yeyote mwenyesilika za ukiukwaji wa haki za binadamu zikiwemo za
namna hii za kuwashambulia waandishi anakwenda kinyume cha wajibu wake nayeye
mwenyewe anavimelea vya uhalifu’’Aliongeza Kibanda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni