Timothy Marko.
SERIKALI ipokatika mkakati wa kuzungumza na nchi ya Burundi ilkujenga reli yakati ambapo ujenzi huo wa reli hiyo utanzia mkoani kigoma katika kata ya uvinza hadi Burundi ambapo ujenzi wa reli hiyo unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana Naibu waziri wauchukuzi Charles Chizeba amesema kuwa ujenzi huo umekuja katika harakati za serikali katika kuboresha biashara katika nchi zilizopo katika ukanda wa wa afrika mashariki ilikuchochea uchumi katika sekta ya miundo mbinu ikiwemo reli.
‘’Tanzania imengia majadiliano na serikali ya Burundi katika ujenzi wa reli unaoanzia kigoma hadi katika nchi ya Burundi ‘’Alisema Charles Chizeba
Katika hatua nyingine Naibu waziri chizeba amewataka wa fanyakazi washirika lareli kuvuta subira juu ya madai yao ya nyongeza ya mshahara ilikuwaidaiwa nawafanya kazi wa shirika hilo la reli nchini.
Naibu waziri Chizeba alisema Baadhi yawafanyakazi walio kuwa wamestahafu kuondoka katika shirika hilo nakuchukua mafao yao ambapo alisisitiza kuwa kitendo cha wafanyakazi hao kurudi kazini nakuendelea kufanya kazi katika shirika hilo nikinyume cha sheria .
‘’naomba watu waliostaafu wachukue mafao yao nakulipwa mafao yao kitendo chakurejeshwa kazini kuendelea kufanya kazi katika shirika hili nikinyume cha sheria ‘’Aliongeza Waziri Chizeba.
Aidha Chizeba, alisisitiza kuwa serikali ipo katika mkakati wa kurejesha masoko yaliyopo katika kila kituo ilkuboresha huduma zilizopo katika vituo mbalimbali vilivyopo pembezoni mwa kituo hicho .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni