Timothy Marko.
JESHI la
polisi nchini kitengo cha uwanja wandege kinamshikilia raia wa vietinam Dong
Van (47)kwa kukutwa na nyara za serikali ikiwemo meno ya simba (65) ikiwemo pia
na kucha za mnyama huyo zipatazo 447 vyenyethamani milioni 189,420.
Akizungumza
na waandishi wa wahabari jijini leo,Kamishinamsaidizi wa polisi Hamis Seleman
amesema kuwa Raia huyo wa vietinam alikutwa na jeshi lapolisi akiwa katika
harakati za kusafirisha nyara hizo za serikali kwa kutumia ndege ya shirika la
Qatar Airways ilikuzipeleka nchini vetinam kupitia Doha
.
‘’Raia huyu
DONG VAN alikutwa na hati yakusafiria yenye namba za usajili B.9306216
iliyotolewa nchini vietinam ambapo raia huyu alikamatwa julai 30 mwaka huu saa
kumi jioni akiwa katika eneo la kuondokea abiria katika uwanja wandege
wakimataifa wa Julius Nyerere’’Alisema Hamis selemani .
Hamis
selemani alisema kuwa baada ya jeshilo lapolisi lililopo katika uwanja huo
wakimataifa wa mwalimu nyerere kufanya upekuzi ndipo raia huyo alikutwa na meno
ya simba (65)na kucha (447 )akiwa amaficha kwenye pakiti saba za kahawa namoja
ilikutwa ina mchele aina ya pure Basmati ikiwa imechanganywa napakiti 15 za
vyakula aina mbalimbali ambazo ziliwekwa kwenye begi la nguo .
Kamishina
msaidizi wa jeshi lapolisi katika viwanja hivyo Hamis seleman alisema kuwa
jeshi lake bado linaendelea na uchunguzi wa raia huyo wa vietinam nakisha
ukikamilka atapelekwa mahakamani .
‘’Uchunguzi
wa kukamatwa kwa raia huyu unaendelea na atapelekwa mahakamani pindi uchunguzi
utakapo kamilika ‘’Aliongeza Kamishina wa uwanja wa ndege wa mwalimu Julius nyerere
.
Katika hatua
nyingine kamishina huyo ametoa wito kwa wananchi kulinda rasmali za nchi popote
walipo ilikuokoa rasmali za taifa na pia kuweza kutoa ushirikiano kwajeshi hilo
pamoja navyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni