Timothy Marko.
Katika kuhakisha sekta ya mawasiliano inakuwa nchini kampuni za mawasiliano ya simu za tigo ,aitel,pamoja na zantel zimeingia makubaliano ya pamoja katika kutuma na kupokea fedha kwa tumia huduma za kifedha zilitolewazo na makapuni hayo amambazo ni Tigo pesa ,Aitel money,na ezypesa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini,Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya tigo Diego Guterrez amesema kuwa ushirikiano huo umekuwa niwakwanza katika bara la afrika ambapo unawezesha wateja wakampuni tofauti za simu kuweza kutumiana nakupokea fedha mojakwamoja kutoka kwenye akaunti zao za simu tofauti.
‘’Ushirikiano huu ni wakwanza barani afrika ambapo unawawezesha wateja wa kampuni tofauti za simu kuweza kutumiana na kupokea fedha moja kwamoja kutoka kwenye akaunti zao za simu tofauti’’Alisema Diego Guterrez.
Diego Guterrez alisema hapo awali kulikuwa nahuduma miongoni mwa makampuni yasimu ambayo yalimuwezesha mteja wamtandao tofauti kuweza kutumianaujumbe mfupi miongoni mwa wateja .
Aliongezakuwa kupitia hudumahiyo ambayowameianzisha itawawezesh awateja wakampuni hizo kuweza kutuma nakupokea pesa kutoka kwenye simu zao moja kutoka kwenye makampuni hayo.
‘’Ushirikiano huu wa wateja wa kampuni hizi tatu wateja watakuwa na uwezo wakutuma pesa kupita simu zao moja kwamoja hii nikwamujibu wa taarifa yapamoja kutoka kwenye makampuni hayo’’aliongeza Guterrez.
Kuhusiana kuboresha huduma zenyeubunifu Mkurugenzi wa kampuni ya mawasilano ya Airtel Sunil Colaso amesema kuwa shirika hilo la mawasiliano nchini limelenga kuwapa huduma zenye ubunifu wa hali yajuu bila kujali ushindani wa kibiashara nakusisitiza kuwa,lengo nikuwapa fursa ya kutuma nakupokea fedha kupitia mitandaohiyo.
‘’ushirikiano huu waleo utawaleta wateja karibu zaidi nahuduma za simu kwakurahisisha matumizi yao yakutuma na kupokea fedha.’’aliongeza colaso.
Kwa upande wake mkurugenzi wa zantel Pratap Ghose alisema kampuni hiyo inayo dhamira ya dhati katika kuhakikisha thamani na ubunifu wa huduma zake kwa sababu kampuni hiyo imefurahishwa na ushirikiano huo ambao utawezesha kufanya bishara kiufanisi.
‘’zantel inajivunia kuwa kampuni yakwanza yasimu iliyoanzisha huduma za malipo yafedha kwanjia yasimu za mikononi tangu mwaka 2008 hivyo itazidi kushirikiana na mamlaka husika ilikuhakikisha tunatoa huduma bora zaidi kwawateja wetu’’Aliongeza Ghose.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni