Jumatatu, 2 Juni 2014

KAMPUNI YA TIGO YA WAKWAMUA VIJANA NA TATIZO LA AJIRA NCHINI

Timothy Marko
 Katika kuboresha huduma za ke kampuni ya simu ya tigo nchini imeingia makubaliano na kampuni ya Dar Teknohama  Bussiness Incubator ilikuwawezesha washiriki wa teknohama kukuza vipaji vyao kupitia mpango maalumu wa mafunzo yakibiashara ambayo itawawezesha kukuza sekta ya ajira nchini  kupitia taluma ya teknohama.
Akizungumza jijini leo katika makao makuu ya Tume ya sayansi na Teknolojia ,Mkurugenzi Mkuu wa Tigo nchini Diego Gutierrez amesema kuwa ushirikiano wa kampuni ya DTBina kampuni yake utwawezesha watanzania ambao ni wanasayansi wa badaye kuweza kupatafursa yakujifunza nakuendeleza biashara zao huku sekta hiyo ya Tehama nchini ikiendelea kukuwa.
‘’hadi sasa teknohama imechangia asilimia 2.3katika GDP ya nchi ,tigoina dhamira ya dhati katika kuhakikisha kiwango hiki kinakuwa kuptia uwekezaji wa rasmali watu ,kwa sababu hii kupitiaDar  tenknohama business incubar (DTB)tunatoa ahadi ya kuwasomesha watanzania 10katika ngazi ya shahada ya uzamili kila mwaka ,pamoja nakutoa mafunzo nakutoa nafasi ya ajira kwa wale watakao jikikta katika masomo Teknohama’’Alisema Gutierrez.
Gutierrez alisema hii inaendana sambamba na malengo ya millennia ya mwaka 2015 (MDG’S )na sera ya Tanzania ya tenknohama ya mwaka 2013 nakuongeza upeo na ufahamu wa masuala ya teknohama katika jamii ya watanzania kwahiyo tunayofuraha kuungana naserikali ili kutoa mchango wetu katika kulifanikisha hili.
Utiliaji saini wa ushirikiano huu ulishudiwa waziri wasayansi Mawasiliano na teknolojia DK Makame Mbarawa ambaye ali ipongeza tigo na kampuni ya DTBikwa kuingia katika ushirikiano serikali inayo furaha ambao utwawezesha vijana wajasilia mali wa teknohama kupata maarifa pamojana msaada wakukuza ubunifu iliwaweze kushindana katika soko la biashara siku za usoni.
DK Makame  Mbarawa alisema kuwa anaamini siku zausoni ushirikiano huo utaweza kutoa fursa kwa vijana katika kupata ajira kwa njia yakuonesha ubunifuwao nakuwa wezesha vijana hao kujipatia kipato.
‘’Napenda kuipongeza Tigo ,DTBi,na COSTECH,kwakushirikiana kwao kutweza kukuza teknolojia na kutengeneza thamani kubwa yabiashara za aina yake kwa vijana’’Alisema Mbarawa.
Akizungumza katika uzinduzi wa ushirikiano huo afisa Mtendaji mkuu wa DTBi mhandisi George Mulamula alisema kwamba ushirikiano huo utawapa fursa ya kuonesha vipaji vyao kitaifa nakimataifa.
Alisema kuwa uzinduzi wampango huo unalenga utamaduni wa ujasiliamali wa teknohama pamoja nakuongeza ajira katika  wigo waubunifu wa teknolojia .
‘’tuligundua yakwamba washiriki wetu walikuwa wamekosa uzoefuwa teknolojia na mazingira yakufanyia biashara ambao ungeweza kuwa nufaisha kuwa wajasiliamali bora zaidi ‘’alisema muhadisi Mulamula.
Mkurugezi Mkuu wa COSTECH DK.Hassan Mshinda alisema kuwa ushirikiano huo kati ya tigo na DTBi unaenda sambamba na dira ya tume hiyo katika kuendeleza uchumi wa taifa kupitia kuaji wa maarifa.
Dk.Hassan Msinda alisema utafiti na maendeleoya teknolojia pamojana ubunifu nikwajili yamaendeleo ya nchi ya Tanzania .
‘’ubunifu huu nikwajili ya maendeleo ya teknolojia pamoja na maendeleo ya tanzania’’alisema Msinda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni