Jumanne, 29 Aprili 2014

LHRC KWAKUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA UJERUMANI LAZINDUA MRADI WA KAZI ZA STAHA KWA WANANCHI WALIOPO KATIKA SEKTA ISIYO RASMI

Timothy  Marko.
Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC)kwakushirikiana na washirika wake DSW ( Deutche stiftung weltbevolker )shirika  laujerumani linalohusiana naidadi ya watu ulimwenguni limezindua mradi wa kazi za staha kwa wananchi walijiajiri katika sekta zisizo rasmi  ilikuwawezesha kupata tija  katika shughuli zao .
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijijni ,Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu  Hellen kijo Bisimba  amesema kuwa mradi huo umekuwa kiendeshwa katika halma shauri tatu zilizopo kanda ya kaskazini ambazo ni Meru ,Arusha na Babati .
‘’mradi huu ambao unafadhiliwa na umoja wa ulaya ambapo ulianzishwa mwaka 2011 umekuwa ukiendeshwa katika halimashauri tatu zilizopo kanda ya kaskazini ambazo ni  Meru ,Arusha pamoja na Babati ‘’alisema Hellen kijo .
Hellen kijo alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake mradi huo umekuwa niwenye mafanikio makubwa ambapo vikundi 36 vya wanawake 20 na vijana 16 kutoka katika vikundi vya wanawake zaidi ya kina mama 620 nakutoka vikundi vya vijana zaidi ya vijana 175 wamenufaika na mradi huo.
Alisema kuwa kituo chasheria na haki za binadamu kimeweza kuwa jengea uwezo wajasliamali hao  kwa kukuza uelewa wa haki za binadamu ikiwemo haki na wajibu wataratibu zakisheria katika usajili na leseni za biashara ,na maeneo muhimu ambayo yameboresha shughuli muhimu zakitaifa kama mchakato wa katiba .
Aidha katika hatua nyingine Bi hellen kijo ametoa mapendekezo kama wakilishi wakikuo hicho kuwa serikali iunde mamlaka itakayoweza kusimamia nakuthibiti taasisi za mikopo zenye riba kubwa ,
‘’watunga sera waweze kutunga sera mahususi zitakazo weka misingi ya sekta zisizo rasmi na mustakabali wake kwani kwa sasa zinaajiri takribani asilimia 60’’aliongeza  hellen kijo.FACEBOOK

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni