Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DK.JONH pombe Magufuli |
Wakati
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) likijipanga kuikatia umeme Zanzibar
kama alivyoagiza Rais John Magufuli, SMZ inajipanga kuzungumza na
shirika hilo ili kuona namna ya kulipa.
Alipotafutwa
kwa simu jana kuzungumzia utekelezaji wa agizo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa
Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema yupo safarini na hakuzungumza kutokana
na mawasiliano kuwa mabaya.
Baadaye mwandishi wetu alimtumia ujumbe mfupi, lakini Dk Mwinuka hakujibu.
Baada
ya kukwama kupata maelezo ya Dk Mwinuka, mwandishi wetu alimtafuta kwa
simu, Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji ambaye alisema
shirika hilo litatekeleza agizo la Rais kama alivyoagiza. “Rais ametoa
kauli na kuagiza… lazima tutekeleze,” alisema Muhaji ambaye hakubainisha
siku ya kuanza utekelezaji wa agizo hilo.
Hata
hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ, Mohamed
Aboud Mohamed alipoulizwa kuhusu deni hilo, alisema wamejiandaa kufanya
mazungumzo kati ya mawaziri husika wa pande mbili za Muungano kuona
namna wanavyoweza kufanikisha ulipaji wa deni hilo.
“Lengo
letu ni kulipa deni lote kwa sababu ukidaiwa lazima ulipe. Tupo tayari
kulipa ndiyo maana tumeanza kufanya mazungumzo na wenzetu wa Tanzania
Bara, ili kuona namna tunavyoweza kukubaliana juu ya Shirika la Umeme
Zanzibar (Zeco) kulipa hatua kwa hatua ili kumaliza deni lote,” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni