Ijumaa, 10 Februari 2017

WATANZANIA WAASWA KUKUZA UTAMADUNI ,WAASWA KUTOVUNJA MISINGI .

Tokeo la picha la BALOZI WA IRANI NCHINI TANZANIA
BALOZI WA IRANI ALI BAGHERI  AKIWA NA MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA SAMIA HASSANI.
Timothy Marko.
KATIKA Kuhakikisha Tanzania inakuwa katika nyanja mbalimbali kimataifa nakukuza utamaduni wake  Watanazania wameshauriwa kukuza utamaduni unaozingatia Maadili mema unaozingatia Misingi ya haki za binadamu .

Hayo yamesemwa na Balozi wa Irani Nchini Tanzania Ali Bagheri wakati akifungua maonesho yasiku ya utamaduni wa Tanzania jijini Dar es salaam  na Irani ambapo amesema kuwa uhusiano wa utamaduni kati ya nchi yake ni wakipindi kirefu tangu enzi za chama cha Afro shirazi kilicho waunganisha watanzania na watu wairani huko zanzibar katika harakati za ukombozi wakisiwa hicho .

''Utamaduni wa Shirazi ama washirazi umejengwa katika misingi yandoa ambapo baadhi washirazi waliweza kuoana nakuweza kuleta jamii mbalimbali ikiwemo wazanzibar ambapo katika misingi ya ndoa za washirazi ndipo uhusiano wa kati ya Tanzania na Irani uliweza kuibuka ''Alisema Balozi Ali Bagheri .

Balozi Bagheri alisema washirazi wengi waliweza kuishi katika mikoa mbalimbali ya ukanda wa pwani wakijishughulisha nashughuli mbalimbali ikiwemo uvuvi hali iliyochangia kukua kwa biashara katika ukanda wa afrika mashariki .
Alisema ni vyema wananchi wa katambua umuhimu mkubwa wakutunza tamadunizetu badala yakuwa watumwa watamaduni baina nchizo mbili kwanzi kukemea vitendoviovu kwa wale  wanao husika katika kukuza uchumi.

Msaidizi wa Kituo cha Mawasiliano cha ubalozi wa irani Fatuma Ali amesema kuwa Wananchi wa irani walipokuwa katika  ukanda wa pwani ya Zanzibar waliweza kujenga misikiti na baadhi ya Majengo ambayo sasa ni magofu hali iliyowezesha kuweka kumbukumbu za majengo ya kale katika eneo hilo .
Alisema kuwa Katika tafiti zilizofanywa zilionesha kuwa asilimia sitini yamaneno yakiswahili yametoka nchini irani hali ambayo inaonesha kuwa nikichocheo muhimu wa lugha yakiswahili katika kukuza utamaduni wa Mtanzania .
''Baada ya tamasha hili kuoneshwa hapa  Dar es salaam ,Tunatarajia kufanya tamamasha kama hili katika mikoa ya Tanzania Visiwani Ikiwemo zanzibar ''Alisema Fatuma Ali

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni