Jumatatu, 6 Februari 2017

REDIO TIMES YAMUUNGA MKONO UMMY MWALIMU DHIDI YA UKATILI .

Tokeo la picha la ummy mwalimu
Timothy Marko .
Kituo cha Redio jijini Dar es salaam  cha Times fm 100.5 kimeanzisha Progamu maalumu yakuielimisha jamii juu ya ukatili wa wa kijinsia kwa wanawake baada ya vitendo hivyo kushamiri nchini .

Akizungumza na Wandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Kituo hicho Luhele Nyaulawa amsema kuwa uanzishwaji wa programu ya uelimishaji wa jamii kupitia vipindi vya Redio kunafuatiwa na kituo hicho kutambua juhudi malimbali za serikali ya kutokomeza janga hilo .

''lengo la Programu hii ni kuunga mkono serikali juu yakutokomeza vitendo vya ukatili wakijinsia hasa kwa wanawake nawatoto vipindi hivi vitarushwa kuanzia kesho kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa sita mchana ''Alisema Mkurugenzi Luhele Nyaulawa .

Katibu Mkuu wa wizara ya Afya Maendeleo ya jamii,Jinsia na Wazee na watoto Sihaba Nkinga amesema kuwa  Tatizo la Ukatili nikubwa nchini ambapo katika takwimu zilizopo 2015 zilizotolewa na jeshi lapolisi jumla yamatukio 3444 ya liweza kutokea katika kipindi hicho ikijumuisha matukio yashambulio ,kujeruhi na matusi vilikuwa ni 14,561 .

Alisema kati yawanawake walio kati ya umri wa miaka 15 -49 waliweza kufanyiwa vitendo vyaukatili wakijinsia ikiwemo shambulio kati yao wasichana asilimia 72 walifanyiwa ukatili wa vipigo .



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni