MENEJA BIASHARA NA MAUZO DSE PATRICK MUSUSA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHANI) JIJINI DAR ES SALAAM JUU YAKUJITOKEZA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KATIKA SHINDANO LA SCHOLLAR INVESTMENT CHALLANGE LINALOTARAJIA KUANZA FEBUARI MOSI MWAKA HUU. |
SOKO lahisa jijini Dar salaam( Dse)limesema kuwa kiwango cha wanafunzi wa vyuo vikuu wanao jiorodhesha katika shindano la soko hilo lijulikanalo kama schollar investment Challange kimezidi kuongezeka mwaka hadi mwaka ambapo hadi kufikia mwaka jana wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali 3200 wameza kushiriki shindano hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Meneja Mauzo na Biashara wa Soko hilo Patrick Mususa amesema kuwa Tangu shindano hilo lianzishwe shindano hilo limeweza kupata mwitikio mkubwa ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wameweza kupata elimu ya biashara na uwekezaji.
''Hadi hivi sasa tangu lianzishwe nimara yanane vyuo vikuu vimekuwa namwitikio mkubwa katika shindano letu,hivyo basi nimaranyingine tena tunawataka wafunzi wengi wavyuo vikuu kuweza kujitokeza ''Alisema Meneja Mauzo na Biashara Patrick Mususa .
Meneja Biashara na Mauzo Mususa amesema kuwa shindano hilo ambalo kwa mwaka huu linatarajia kuanza February Mosi anatarajia kuwepo kwa ushindani mkubwa kutokana baadhi yavyuo kutarajiwa kuongezeka na kuweza kukuza ushiriki wao.
Katika hatua nyingine Soko hilo limesema kiwango cha hatifungani kimepanda kutoka shilingi bilioni 15.7 hadi kufikia shilingi 24.2 bilioni hali iliyochagiwa na hati fungani tisa za serikali zenye thamani ya shilingi 24.2 bilioni ziliweza kuuzwa katika kipindi cha mwezi january .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni