Jumanne, 24 Januari 2017

CCM YAAHIDI KUFANYA SIASA ZA MAENDELEO 2020.

Tokeo la picha la humphrey polepole


Timothy Marko .
Chama cha Mapinduzi nchini CCM kimesema kuwa kitajikita katika katika siasa za maendeleo na kuwaletea wananchi maendeleo ifikapo mwaka 2020 ilikuweza kushindana vyama vya upinzani nchini .





Akizungumza na waandishi wa Habari katibu Mwenezi wa Chama hicho Humprey Polepole amesema kuwa lengo lachama hicho nikuhakikisha inawapata viongozi waadilifu watakaleta ushindani katika uchaguzi.

''tutaendelea kushirikiana na wananchi katika kutatua kero zao naninawataka viongozi waCCM Kuendelea kuwa wadilifu kwani uchaguzi ujao wa mwaka 2020 unalenga kuwaletea viongozi wa adilifu watakao waletea maendeleo wananchi ''Alisema Humprey Polepole .

Polepole alisema kuwa katika mkakati uliopo wachama hicho wanalenga kutenga asilimia 20 ya mapato yao kwajili kuwaendeleza vijana na wanawake ilikuweza kujiajiri na kuajiriwa ilkuweza kupunguza tatizo la ajira .

Alisema katika hatua yakuelekea uchumi waviwanda chama hicho kitaihimiza serikali kuweka ulinzi katika viwanda vyandani iliviweze kuzalisha nakukuza ajira kwa vijana .
''Tutahakikisha tunaziba mianya yote RUSHWA  ndani yaserikali ,utafiti unaoneshakuwa  wananchi wamekuwa wakiridhishwa nakasi yetu katika kudhibiti ufisadi na rushwa ,tutahahikisha kodi zote zinalipwa nakuziba mianya yaukwepaji kodi ''Aliongeza Polepole .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni