Mkurugenzi MTENDAJI wa Rahaco MASANJA KADOGOSA akizungumza na waandishi wa habari juu ya uboreshaji wa miundombinu ya Reli NCHINI . |
Serikali imesema zaidi yaDola za kimarekani bilioni 7.683 zitatumika katika ujenzi wa Reli kwa kiwango cha Standard gaugeilikuweza kkukamilisha mtandao wa reli wa nchi nzima wenye urefu wa kilometa 2,561.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Kaimu Mkurugenzi wa Rahaco Masanja Kadogosa amesema kuwa ujenzi wamradi huo utakuwa ni wa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza itajumuisha Isaka mwanza kilometa 1219 ambapo jumla yashilingi biloni 3.694 zitatumika katika kukamilisha mradi huo.
''Awamu yapili itakuwa Tabora -uvinza ,kigoma km411 ambapo zaidi ya bilioni 6.7145 isaka -rusumo km371 ,keza -ruvubu (km36 bilioni 4,926 wakati uvinza hadi kalema hadi msogati km203 ambapo bilioni .053 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo ''Alisema kaimu Mkurugenzi Masanja Kadogosa .
Kaimu Mkurugenzi wa Rahaco Kadogosa alisema kuwa zoezi la utekelezaji wa miradi hiyo utajumuisha hatua mbalimbali ikiwemo usanifu hadi hatua za kumpata mkandarasi wa ujenzi wa miradi hiyo ambapo miradi hiyo ininataraji wa kukamilika baada ya miaka mitatu ambapo awamu yakwanza yaujenzi huo itanza Dar es salam hadi mwanza .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni