Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni 
Ali Salum Hapi ametoa tahadhari kwa wahusika waliofanya ubadhilifu 
katika kuwapatia pesa za misaada ya Tasaf kwa wasiostahiki na 
kusababisha upotevu wa fedha za serikali. Hayo ameyasema leo katika 
mkutano wake na Waandishi wa Habari akidai kuwa wote waliopata fedha 
hizo wanatakiwa wazirudishe  mahala stahiki ili zifanyiwe kazi kwa 
wanaostahiki.
Hapi amesema Tasaf na pesa 
zilizotolewa zilikuwa kwa ajili ya kuwasaidia kaya zilizo na hali mbaya 
kiuchumi ili ziwasaidie kupata nguo  za shule pamoja na huduma nyingine 
za kijamii, hivyo udanganyifu uliofanyika umebaini kaya hewa 566  pia 
kaya nyingine 265 na kaya nyingine 59 zote za Wilaya ya Kinondoni pamoja
 na kaya zilizobaki wamehama maeneo hayo hivyo kuna fedha zinachukuliwa 
na haijulikani wapi zinaenda baada ya kubaini na kufanya uchunguzi wa 
fedha hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni