Timothy Marko .
Uwezo wanguvu yasoko umetajwa kuwandio unaoathiri kwakiasi kikubwa mauzo ya soko lahisa kupanda kwa asilimia 28 kwawiki hii ambapo mauzo ya hisa yameweza kupanda katika soko la Dar es salaam (DSE) Kutoka bilioni 3.hadi kufikia bilioni 3.8 kwawiki hii.
Hayo yamebanishwa leo na Afisa mwandamizi wa Soko lahisa la Dar es salaam Mary Kinabo wakati akizungumza na waandishi wahabari juu ya mabadiliko ya bei yahisa sokoni hapo ,ambapo aliitaja Benki ya CRDB ikiongoza kwa kuuza hisa zake kwa asilimia 95.18 ikifuatiwa Mwalimu Commerical Bank kwa silimia 2.92 huku TBL ikishika nafasi yatatu kwa asilimia 079
''Ukubwa wa mtaji umeweza kupanda kwa asilimia3.53 kutoka trioni 20.8 hadi trioni 21.56 wakati mtaji wa makampuni ya ndani umepanda kwa asilimia 0.36 kutoka trioni8.13 hadi 8.16 ''Alisema Afisa Mwandamizi Mary Kinabo .
Kinabo alisema kuwa sekta yaviwanda kwa wiki hii imeweza kupanda kwa pointi 26.16 baada ya kupanda kwa bei yahisa za TBL kwa asilimia 0.76 ikilinganishwa na sekta yahuduma za kibenki ambayo imeonekana kushuka kwa pointi 0.51 baada hisa katika kaunta ya soko hilo kushuka kwa asilimi3.13 .
Alisema kuwa sekta yahuduma zakibiashara kwa wiki hii imeweza kubakia kiwango kilekile cha shilingi 3534.64 baada ya swisport kutobalidika katika kiwango cha awali .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni